Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kimbunga chabomoa nyumba 21 Rukwa
Kimbunga chabomoa nyumba 21 Rukwa
By Habari Tanzania | Published  01/18/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Doris Mageta, Sumbawanga

NYUMBA 21 zimeezuliwa mapaa na nyingine kubomoka pamoja na mtu mmoja kujeruhiwa kutokana na kimbunga kikali kilichotokea jana mchana katika Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.

Kimbunga hicho kilianzia majira ya saa 8.30 mchana eneo la Kata ya Katandala na kuelekea katika mtaa wa Kristu Mfalme na kuishia katika eneo la Msitu wa Mbizi.

Katika sehemu zote kilikopita kimbunga hicho, kiliezua na mapaa ya nyumba na kuyaharibika, kubomoa nyumba moja, kuharibu mali mbalimbali za watu na kumjeruhi mkazi mmoja wa nyumba iliyobomoka.

Hata hivyo, dakika chache baadaye mvua kubwa ilinyesha na kusababisha waathirika wa kimbunga hicho kuanza kuhangaika, kuhifadhi vifaa vyao ili visiharibiwe na mvua hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel Njoolay jana aliwatembela wahanga hao wa kimbunga kuwafariji na kuwaeleza kuwa serikali mkoani hapa inaandaa utaratibu wa kuwasaidia kwa hali na mali.

Alisema serikali imeaanda harambee itakayofanyika January 19 katika ukumbi wa Libori kwa ajili ya kuwasaidia wahanga hao wa kimbunga na kuwataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa hususan Manispaa ya Sumbawanga kujitokeza kwa wingi katika harambee hiyo.

Njoolay aliwataka wafanyabiashara wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kwa kuleta fedha na vifaa mbali mbali vya ujenzi kama mabati na mbao, ikiwa njia moja wapo ya kuwasaidia wananchi walioathirika na janga hilo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.