Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Baada ya mgawo sasa umeme wa kumwaga Tanzania
Baada ya mgawo sasa umeme wa kumwaga Tanzania
By Habari Tanzania | Published  01/18/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Ramadhan Semtawa

UZALISHAJI umeme nchini ulioingizwa katika gridi ya taifa umeongezeka kwa kiwango kikubwa hadi kufikia megawati 926 kwa sasa.

Kiwango hicho ni cha juu ikilinganishwa na mahitaji halisi ya juu ya umeme nchini ambayo ni megawati 578.

Wakati umeme uzalishaji ukiongezeka katika kiwango hicho, kiwango cha maji katika bwawa la Mtera nacho kinakariba kufikia katika ujazo wa kawaida kwani hadi sasa bado mita 3.5 juu ya usawa wa bahari.

Ingawa bwawa hilo limebakiza mita za chache za ujazo kufikia katika kiwango chake cha kawaida cha maji ambayo ni mita 696.8 juu ya usawa wa bahari, hadi sasa halijaanza kuzalisha umeme, kwani limewekwa kama akiba ya baadaye.

Katika kipindi cha mwaka jana Tanzania ilikumbwa na ukame uliosababisha upungufu mkubwa wa nishati ya umeme hali iliyosababisha serikali kutafuta umeme wa dharura ambao hadi sasa zimefungwa megawati 62.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, wakati akifungua mkutano wa wakilishi wa nchi zinazounganishwa na miradi ya bonde la mto Nile (NIB), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, William Ngeleja, alisema ongezeko hilo la uzalishaji umeme limekuja wakati tayari Tanzania ilikwishapita katika kipindi kigumu cha ukame.

Karamagi alisema nchi hizo zinapaswa kufahamu changamoto zinazokabili ukanda huo katika suala zima la uzalishaji nishati ya umeme ambazo ni pamoja na ukame.

Waziri Karamagi alisema wataalamu kutoka nchi hizo za bonde la mto Nile wanapaswa kuibua na kuendeleza miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia mbinu mpya zaidi ili iweze kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya nchi hizo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Arthur Mwakapugi, alisema hadi sasa kuna miradi nane tofuati ikiwemo ya uzalishaji umeme inayoendelezwa katika ukanda huo.

Mwakapugi alifafanua kwamba, kwa Tanzania mradi unaendelea kutekelezwa ni wa uzalishaji umeme kwa kuunganisha na nchi jirani ya Rwanda.

Mpango wa maendeleo wa bonde la Mto Nile ulianza mwaka 1999 baada ya mawaziri kutoka nchi kumi ambazo ni Tanzania, Rwanda, Kenya, Uganda, Misri, Ethipia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Uganda, Sudan na Eritrea.

Utekelezaji wa miradi ya NBI ambayo ni pamoja na kilimo, uzalishaji umeme na shughuli nyingine za kiuchumi kutoka nchi fadhiri.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Activeman)
    Rating
    Hanuna cha kusherekea hapa, haya ni matatizo juu ya matatizo.

    Hapa ndiyo ujue kuwa zile siasa walizokuwa wanaongea kuanzia waziri mkuu, rais, waziri wa nishati zilikuwa ni blah blah tupu. hawakujua tatizo ni nini hasa la mgao wa umeme. Na kiasi kikibwa ni kwamba watendaji wa wizara ya nishati na Tanesco ni wababaishaji na wanatakiwa kama zi kufutwa kazi basi waombe kazi upya. walishindwa kumpa waziri wao habari za ukweli kuhusu tatizo la umeme. sasa na hii mikataba tuliyoingia je? tuliwahitaji hawa jamaa wa Richmond- Marekani kweli? hii surplus ya umeme tutaipeleka wapi sasa? maana deal ipo hivi = tumia umeme usitumie gharama zipo palepale, mtanzania lazima ulipie huu uozo!!. Hakuna planners kwenye hii wizara au?. Rais haoni au hana vision ya hili kweli, kwanini asitoe tamko rasmi la kuwaweka kiti moto wahusika wote. Au tuseme hawa ndiyo wale wanaotoaka ikulu wakisema wametoka kumwona "our friend JK"
    Maoni: Mpiga kura fumbua mamcho yako!!
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.