Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Askari Magereza sita wadaiwa kumuua mfungwa kwa kipigo
Askari Magereza sita wadaiwa kumuua mfungwa kwa kipigo
By Habari Tanzania | Published  06/14/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Jeshi la Polisi Nchini, linawashikilia askari sita wa gereza la Kimbiji, Kigamboni, Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua mfungwa kwa kipigo.

Askari hao wanatuhumiwa kumuua mfungwa aliyekuwa na namba 180/2006 Eradius Stanslaus ambaye alifungwa jela mwaka mmoja katika gereza hilo.

Marehemu na mwenzake mwenye namba A 422/2006, Gome Christopher, walidaiwa kupigwa na askari hao baada ya kutoroka katika gereza hilo Juni 5, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kapteni (mstaafu), John Chiligati, watuhumiwa hao ni A.9442 Sajini David, A. Koplo Michael, A. 7680 Koplo Rafii, B. 2241 Koplo Abdul, B. 2423 Wdr Heri na B. 3269 Wdr Avith.

Ilisema kuwa, askari hao wamekabidhiwa Jeshi la Polisi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji.

Waziri Chiligati alisema katika taarifa yake kuwa, kufuatia kifo cha mfungwa huyo Juni 6, mwaka huu, Kamishna Mkuu wa Magereza aliunda Kamati kuchunguza mazingira ya chanzo cha kifo hicho.

Alisema uchunguzi ulionyesha kuwa, mfungwa huyo na mtoro mwenzake mara waliporejeshwa gerezani, alifungiwa mahali na kupigwa sana na baadhi ya askari wa gereza hilo.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.