Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mvua yaharibu barabara Tunduma-S'wanga
Mvua yaharibu barabara Tunduma-S'wanga
By Habari Tanzania | Published  01/17/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Stephano Simbeye, Mbozi

WASAFIRI 150 na magari kadhaa yakiwemo ya abiria na mizigo yamekwama katika eneo la Miangarua katika barabara ya Tunduma – Sumbawanga baada ya barabara hiyo kuharibika kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa.

Baadhi ya madereva walimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa iwapo serikali haitafanya matengenezo ya dharura kuna uwezekano mkubwa wa barabara hiyo kufungwa.

Dereva Elieza Mkisi wa gari la Mamlaka ya Hali ya Hewa alisema alilazimika kupitia porini kwa kuwa gari lake lina nguvu, lakini alisikitishwa na kukwama kwa mabasi mawili ya Summry yaliyokuwa na abiria zaidi ya 150.

Naye Mshamu Abdu, dereva wa lori lenye namba za usajili T413 AGY alieleza kuwa tatizo hilo lisipopatiwa ufumbuzi mapema kuna uwezekano bei za bidhaa na nauli kupanda kufuatia ubovu huo wa barabara hiyo.

Akina mama na watoto ndiyo walioathirika zaidi kutokana na kukwama kwa mabasi hayo kwa kuwa hakubeba vyakula kwa kuamini kuwa masaa matatu hadi manne yangetosha kumaliza safari.

Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Rukwa hakuweza kupatikana ili kutoa ufafanuzi juu ya hatua zitazokazochukuliwa

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.