Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wasomi wahimizwa kurudi kwao kuendeleza elimu
Wasomi wahimizwa kurudi kwao kuendeleza elimu
By Habari Tanzania | Published  01/17/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Lilian Lugakingira, Bukoba

UBORESHAJI wa elimu ya msingi na sekondari nchini utaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa endapo wasomi kutoka katika fani mbalimbali, watakubali kurudi nyumbani kwao na kutoa misaada katika shule walizosomea.

Hayo yalisemwa na mfanyabiashara maarufu wa mjini Bukoba, Remigius Patrick, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa madawati 30 yenye thamani ya Sh900,000 kwa shule ya msingi Omukilembo iliyoko Kata ya Bugandika Wilaya ya Bukoba.

Patrick alisema endapo watu hao ambao ana uhakika kuwa wapo wenye uwezo mkubwa kifedha, watakumbuka kurudi kwao na kutoa misaada kama hiyo, wataweza kuondoa matatizo ya upungufu wa madawati shuleni, upungufu wa nyumba za walimu, vyumba vya madarasa na ujenzi wa vyoo.

Alisema misaada mingine pia ya sare za shule, viatu, madaftari, karo na mahitaji mengine muhimu ya shule pia nayo yanaweza kutatuliwa kwa njia hiyo hasa kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo alisema kuwa ameamua kutoa msaada huo kama njia mojawapo ya kulipa fadhira katika shule hiyo aliyosomea na kuwa msingi mzuri wa maisha na mafanikio aliyo nayo ni matunda ya shule hiyo.

Pia mfanyabiashara huyo, aliahidi kuwalipia karo na mahitaji yote ya shule kwa mwaka mmoja wanafunzi wote tisa, waliochaguliwa kuendelea na masomo katika shule mbalimbali za sekondari ili kuwawezesha kuendelea na masomo yao.

Awali akitoa taarifa ya shule hiyo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Donatus Ishengoma alisema shule hiyo ina wanafunzi 332 na walimu nane na kuwa ina upungufu wa madawati 60, ambao alisema zinafanyika jitihada za kila namna ili kuhakikisha madawati hayo yanapatikana.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.