Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Madarasa ya msingi, sekondari hayakidhi viwango- Wabunge
Madarasa ya msingi, sekondari hayakidhi viwango- Wabunge
By Habari Tanzania | Published  01/16/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
NA ELIZABETH MAONI, SUMBAWANGA
 
ASILIMIA 90 ya majengo ya shule za msingi na sekondari mkoani Rukwa, yamejengwa kwa kutozingatia vipimo na ramani vilivyotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imefahamika.
 
Hayo yalielezwa hivi karibuni na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, iliyotembelea mkoani Rukwa kukagua maendeleo ya elimu.
 
Akisoma majumuisho ya ziara ya kamati hiyo, Mwenyekiti wake Mbunge wa Iramba Mashariki, Mgana Msindai alisema majengo mengi hayajafuata vipimo na ramani inayokubalika, hali inayoonyesha kuwa wahandisi hawafiki katika maeneo ya vijijini kukagua ujenzi unavyoendelea.
 
Alisema wilaya ya Nkasi ndiyo inayoongoza kwa kuwa na majengo yaliyojengwa chini ya kiwango, hali iliyoilazimu kamati hiyo kuagiza baadhi ya majengo ya madarasa kubomolewa na kujengwa upya.
 
Msindai alisema Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imejaribu kufanya vizuri.
 
Kamati hiyo imewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa huu kutekeleza maagizo yanayotolewa, ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya Aprili, mwaka huu.
 
Agizo hilo lilitolewa kufuatia kamati hiyo kubaini taarifa za fedha zisizo sahihi za manunuzi ya vifaa vya hospitali ya wilaya ya Mpanda. Zilitofautiana na zilizotolewa awali.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay aliiomba kamati hiyo kuangalia uwezekano wa kukagua miradi ya maendeleo mkoani Rukwa kila mwaka, ili kuongeza kasi ya utekelezaji.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.