Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Tanzania sasa ni kinyozi –Kikwete
Tanzania sasa ni kinyozi –Kikwete
By Juma Pinto | Published  01/14/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
London

Afuta msemo wa kichwa cha mwendawazi
Aona live pambano la Tottenham na Newcastle

RAIS Jakaya Kikwete amesema Tanzania imeondokana na kuwa kichwa cha mwenzawazimu katika michezo na sasa imegeuka kuwa kinyozi.

Rais Kikwete aliyasema hayo, juzi katika mkutano mkubwa wa Tanzania wanaoishi hapa Uingereza katika hotelio ya Chuchill iliyopo Portmond Square katikati ya Jiji na London.

Hayo yalisemwa na Rais kufuatia Kaimu mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania hapa London, Nora Sumari kumpongeza katika juhudu zake za kuinua michezo nchini Tanzania hususani mpira wa miguu.

“Kweli tumejizatiti na hivi karibuni timu yetu ya Taifa inakwenda Brazil kwa mazoezi ya mwezi mmoja na kwenda moja kwa moja kucheza na Senegal, tusubiri tuone hali itakavyokuwa huko,naamini tutashinda” alisema Rais.

Msemo wa Tanzania kichwa cha mwendawazimu ulisemwa na Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kufuatia Tanzania kutofanya vizuri katika michezo mbalimbali, kwa kipindi hicho.

Alisema baada ya kurudi Senagal, timu hiyo itafanya ziara kadhaa ya nchi za Ulaya kabla ya kucheza na Burkinafaso na Msumbiji katika mfululizo wa kuwa nia nafasi ya kucheza fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini Ghana mwakani.

Rais alisema jambo lolote huwezi kufanikiwa kama huna nia, Serikali ya awamu ya nne imehakkikisha kuwa michezo inapiga hatua kubwa na imeanza kwa kasi katika soka, lakini michezo mingine nayo inafuata.

Tanzania sasa inaongoza kundi la saba ya michuano ya awali ya kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika.Tayari imejikusanyia pointi nne kati ya michezo miwili iliyocheza.

Katika mkutano huo uliohudhuliwa na Watanzania wengi hali iliyofanya wengine kuzuiwa kuingia ndani ya ukumbi kutokana na kufurika watu, Rais alikatiza mkutano huo ili kuwahi pambano la Tottenham na Newcastle lililofanyika katika uwanja wa White hate Lane, Edmonton hapa London.

Rais aliwaomba Watanzania hao wa London, kumsamehe kwani alialikwa huko na wenyeji wake, hivyo isingekuwa jambo jema kutokwenda wakati alishakubali na kuahidi kumalizia kiporo hicho katika ziara zijayo.

Katika pambano hilo Newcastle iliweza kuibuka kidedea kwa kuifunga Tottenham kwa mabao 3-2.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by P. S Ole Meelta)
    Rating
    Finally our great country of Tanzania which the most beautiful and we must be proud, got the leader of our destiny.
    Ole-Meelta (GOLF PLAYER)
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.