Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mkuu wa mkoa ataka orodha wanaojaza mimba wanafunzi
Mkuu wa mkoa ataka orodha wanaojaza mimba wanafunzi
By Habari Tanzania | Published  01/15/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Samuel Msuya, Morogoro

KATIKA harakati za kudhibiti upataji mimba kwa wasichana wa shule za msingi, Mkuu wa Mkoa Morogoro, Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo ameagiza kuwa sasa anahitaji kuona idadi ya watuhumiwa waliokamatwa kwa kosa hilo na si idadi tu ya wasichana waliojazwa mimba.

Kalembo alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa kikao cha kujadili maendeleo mbalimbali ya mkoa huo, yaliyofanyika mjini hapo katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Oasis.

Alisema amechoka kusikia maneno ya kuwa wasichana kadhaa wametiwa mimba, hivyo kuwataka wahusika wa sheria waweze kuwachukulia hatua mara moja watuhumiwa wa matukio hayo ambao ni wanaume.

Alisema kuwa kitendo cha kusikia kuwa wasichana wamepewa mimba na watuhumiwa pasipo kuchukuliwa hatua, huchochea vitendo hivyo kuendelea kwani wengine nao huiga baada ya kuona wenzao hawajachukuliwa hatua zozote za kisheria.

Hata hivyo, Kalembo aliwaomba wazazi kuwaandikisha shule watoto wao mwaka huu na kusisitiza kuwa yeyote atakayebainika kutofanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Alisema wazazi ni lazima wahakikishe wanawaandikisha watoto wao na kuwafuatilia kama wanahudhuria masomo ili kudhibiti utoro.

Alisema utoro umekuwa ni sugu kwa baadhi ya watoto mkoani hapa, kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kuwafuatilia kama wanaenda shule na kuhudhuria vipindi.

Mkoa wa Morogoro una idadi kubwa ya washichana wanaopata mimba ambapo kwa mwaka jana, jumla ya wasichana 509 walishindwa kumaliza elimu ya msingi na kujiunga sekondari


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Sarah James)
    Rating
    Kwa kweli ni swala zuri sana kama litafanyika kama alivyoagiza mkuu wa mkoa
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.