Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Karume apongezwa kuwajali wafanyakazi
Karume apongezwa kuwajali wafanyakazi
By Habari Tanzania | Published  01/14/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Salma Said, Zanzibar
Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) Makame Launi Makame, ameipongeza hotuba ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliyoitoa katika kilele cha kuadhimisha miaka 43 ya Mapinduzi na kusema kuwa, imeonyesha nuru mpya kufuatia kugusa vipengele vingi vinavyojali maslahi ya wafanyakazi.

“Tunaipongeza hotuba ya rais Karume, imetupa moyo sana katika utendaji wa shughuli zetu tumeanza kuonekana kama wadau na sio watumishi tena,” alisema.

Aliongeza kuwa, kitendo cha serikali kuanza kuwalipa watumishi wastaafu maslahi yao ikiwemo kiinua mgongo kwa kutenga jumla ya sh.Billioni 3.5 kwa wafanyakazi 1,135 kinaonesha matumaini mapya kwa wastaafu hao.

“Unajua kwa muda mrefu wafanyakazi wanaotaka kustaafu utumishi wao wamekuwa wakijenga hofu kubwa kwa kuogopa kufanya hivyo huku tatizo kubwa ni kutolipwa mafao yao, ” alisema.

Hata hivyo rais Karume alibainisha katika hotuba hiyo kuwa, kuna tatizo la ajira kwa vijana na akaongeza kuwa, moja ya njia ya kuondokana na tatizo hilo ni kuimarishwa kwa sekta ya binafsi kuchukuwa nafasi ya sekta rasmi.

Rais Karume alisema, tatizo kubwa liliopo kwa upande wa Zanzibar ni kwamba serikali imekuwa ndio mwajiri mkubwa huku sekta binafsi ikiwa bado haijachukuwa nafasi yake katika kuajiri wafanyakazi.

Wakati huo huo, Katibu huyo alisema kuwa, kumekuwepo na uvunjifu mkubwa wa haki za wafanyakazi Zanzibar .

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina ya siku mbili ya vyama vya wafanyakazi katika ukumbi wa walemavu, Katibu Mkuu huyo alisema wafanyakazi wengi hawajui haki zao hali inayowafanya kunyanyaswa na waajiri wao, bila wao kufahamu.

Alisema, wafanyakazi wengi wamekuwa wakidhulumiwa mishahara yao huku wengine wakipunjwa kwa kulipwa mishahara midogo jambo ambalo linalindwa na sheria za kazi, sheria zinazobanisha wazi kuhusu viwango mishahara wa kima ya chini.

Akithibitisha zaidi kauli yake hiyo alisema, baadhi ya wafanyakazi wakiwemo walimu wanalipwa 15,000 kwa mwezi na wanashindwa kwenda popote kudai haki zao kutokana na kutofahamu haki zao.

Katibu Mkuu huyo alielezea kuwa, lengo la Shirikisho ni kufanya ziara maalumu katika sehemu za kazi kuangalia wafanyakazi wasiotambua haki zao na kisha kuwasaidia


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.