MAWALIANO kati ya Dar es Salaam na mikoa ya Kaskazini na nchi jirani yaliyokatika katika daraja la Lugoba yamerejea katika hali ya kawaida baada ya kujazwa kifusi katika sehemu ya juu ya daraja jipya.
Magari yaliyokuwa yamekwama katika yalianza kupita juzi jioni kwa kutumia upande mmoja wa daraja kuruhusu kazi ya kutengeneza daraja iendelee.
Mhandisi wa Ujenzi Mkoa wa Pwani, Happyness Mgalula, alisema matengenezo yalifanyika juzi jioni kwa kutengeneza daraja la muda ili magari yaweze kupita.
Meneja huyo amewaondoa wasiwasi wananchi wanaotumia barabara ya Chalinze-Segera kuwa inapitika bila matatizo yoyote baada ya muda mfupi.