Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  ‘Viongozi Sinza wameshindwa kudhibiti uchafu’
‘Viongozi Sinza wameshindwa kudhibiti uchafu’
By Habari Tanzania | Published  12/27/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Agnes Yamo

WAKAZI wa vitongoji vya Sinza, Dar es Salaam, wamelalamika kuwa viongozi wa serikali za mitaa katika eneo hilo wameshindwa kusimamia uchafu.

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti, wakazi wa mitaa ya Hondohondo na Dege, walisema viongozi hao wameshindwa kuwadhibiti baadhi ya wananchi ambao vyoo vyao hutiririsha maji machafu.

Walisema katika kipindi hiki cha mvua, vyoo vingi vibovu na vilivyojaa vinatiririsha maji machafu kuelekea kwenye makazi ya watu na barabarani.

Baadhi ya wakazi wa mitaa hiyo waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini, walisema kuwa viongozi wa serikali za mitaa wanaifahamu hali hiyo na wanawafahamu watu ambao vyoo vyao ni vibovu na vilivyojaa lakini hawawachukulii hatua zozote.

Walisema baadhi ya wamiliki wa vyoo vilivyojaa wamekuwa na tabia ya kutoboa matundu katika mashimo ya vyoo vyao ili kuepuka gharama za upakuaji wa kinyesi kwa kutumia magari ya kuzoa uchafu wa aina hiyo.

“Tabia hii inafanywa na wananchi wenzetu, baadhi wanatoboa matundu kwenye vyoo vyao, kinyesi kinatoka na kuchukuliwa na maji ya mvua, lakini wengine kwa makusudi wanafungua matanki yao na kutiririsha kinyesi ambacho kinachukuliwa na maji ya mvua hadi kwenye makazi ya watu na barabarani.

“Tumelalamika sana kwa viongozi wa serikali ya mtaa wetu, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa, baadhi ya wenye vyoo hivi sasa wanatutukana, wanadai kama tuna uchungu sana tutoe fedha ili yaje magari ya kunyonya kinyesi yaondoe uchafu huo katika vyoo vyao.

“Wasio wastaarabu wanadiriki kutuambia kuwa fedha ya kumpa mwenyekiti wa mtaa ili akae kimya ni kidogo kuliko fedha kwa ajili ya kukodi gari la kunyonya kinyesi, hivyo ni bora kumhonga mwenyekiti wa mtaa kuliko kukodi gari hilo,” alisema mkazi mmoja wa Mtaa wa Hondohondo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

Mkazi mwingine alisema kuwa, tabia hiyo inahatarisha maisha ya wananchi wa Sinza kwa ujumla, hususan watoto wanaopenda kuchezea maji, kwa sababu wanaweza kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na kichocho kwa urahisi.

Alisema kuna baadhi ya nyumba ambazo mvua kubwa ikinyesha maji huingia ndani na wakati wa kuyakausha kina mama wanalazimika kupiga deki kwa kutumia matambala na mikono, jambo ambalo ni hatari kwa afya zao kutokana na maji hayo kuchanganyika na kinyesi.

Wamesema kitendo cha viongozi hao kukaa kimya katika tatizo kama hili kinadhihirisha kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao kwa kuwaacha wananchi katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.