Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Akutwa akining’ inia kwenye nyaya za umeme
Akutwa akining’ inia kwenye nyaya za umeme
By Habari Tanzania | Published  06/12/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Mtu mmoja amekufa na mwili wake kukutwa umening’inia juu ya nyanya ukiwa umekauka mithili ya mkaa baada ya kujaribu kukata nyaya za Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Alfred Tibaigana alisema jana kuwa tukio hilo, lilitokea majira ya saa 10:00 alfajiri, eneo la kiwanda cha vioo Chang’ombe Jijini juzi.

Alisema aliyekufa ni mwanaume ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja na anakadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 25 hadi 30.

Alithibitisha kuwa kijana huyo aliungua hadi kufa wakati akijaribu kuiba nyaya za umeme.

Kamanda Tibaigana alisema wakati kijana huyo anakata nyaya hizo ghafla ulitokea mlipuko mkubwa kutoka kwenye transfoma iliyokuwa karibu na eneo hilo na kumuunguza... alifariki papo hapo.

Aliongeza kuwa mlinzi aliyekuwa akilinda eneo la kiwanda hicho aliposikia mlipuko huo alikwenda eneo la tukio na kumkuta marehemu akiwa amekauka juu ya nyaya hizo na ndipo alipotoa taarifa kituo cha polisi nao waliitaarifu Tanesco.

Katika tukio lingine, Kamanda Tibaigana alisema mtu mmoja amekufa baada ya kuangukiwa na kibanda alichokuwa ndani yake.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4:00 usiku eneo la Mtaa wa Kongo-Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Alisema kibanda hicho kilianguka baada ya gari lenye namba za usajili T 551 AAG likiendeshwa na dereva asiyefahamika likitokea Jangwani kuelekea Msimbazi likiwa katika mwendo wa kasi kukata kona na kumgonga mwenda kwa miguu ambapo baadaye liligonga kibanda hicho ambacho kilikuwa na zege lililomwangukia mtu huyo na kumsababishia mauti.

Katika tukio la tatu, kamanda huyo alisema mtu mmoja alikufa baada ya gari alilokuwa akisafiria kuacha njia na kugongana uso kwa uso na gari lingine.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi katika barabara ya Chekeni Mwasongwa eneo la Kisarawe 2 wilaya ya Temeke Jijini.

Alisema ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T 955 AAM, Toyota Corrola likiendeshwa na Said Majid (35),lililokuwa likitokea Kisarawe 2 kuelekea Kibada, kuacha njia na kugongana na gari lenye namba za usajili T 659 ALV, Nissan Pick-Up likiendeshwa na Bw. Peter Novat (40).

Aidha alisema abiria aliyekuwa kwenye gari namba T 955 AAM, Nasra Masoud (70) alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.