Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wananchi wamlalamikia DC Temeke
Wananchi wamlalamikia DC Temeke
By Habari Tanzania | Published  12/22/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mobini Sarya

WAKAZI wa Kata ya Somangira wilayani Temeke, Dar es Salaam, wamemlalamikia Mkuu wa Wilaya (DC), Abdallah Kihato, kwa kushindwa kufanya mkutano wa hadhara na kusikiliza kero zao.

Wakazi hao wameiambia Tanzania Daima kwamba, viongozi wao walikuwa wamewatangazia kuwa, Kihato angefika kwenye kata yao kujitambulisha na kufanya mkutano wa hadhara.

“Walipita mitaani wakituambia siku hiyo tujitokeze, mwenye kero amweleze DC mpya, tena tufike mapema saa tano, na kweli wananchi tukaacha kazi zetu, tukajitokeza siku hiyo, hata hivyo mkuu huyo alikuja saa saba mchana,” alisema mzee Mpema, mkazi wa Somangira.

Alidai kuwa, baada ya mkuu huyo kufika, viongozi wa kata walimpokea na kwenda kukaa naye kwenye ofisi zao hadi jioni.

Mzee Mpema, alisema wananchi waliendelea kuvuta subira wakidhani kuwa mazungumzo yao yatamalizika mapema ili awahutubie kwenye mkutano wa hadhara bila mafanikio.

Alisema bila shaka viongozi hao walifanya hivyo makusudi ili DC huyo asipate nafasi ya kuzungumza na wananchi kujua maovu yao.

Alipoulizwa na Tanzania Daima kwa njia ya simu, kuhusu kero hizo, DC huyo alisema wananchi hao wanalaumu, lakini hawakujua ratiba yake.

“Ziara yangu ilikuwa ni ya kuongea na maofisa maendeleo wa kata zote, sio kusikiliza kero za wananchi, ipo siku nitafanya hivyo, kule ni eneo langu l


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.