Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Dodoma yapongezwa
Dodoma yapongezwa
By Habari Tanzania | Published  12/21/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Jamal Zuberi, MAELEZO- Dodoma
 
RAIS Jakaya Kikwete amewapongeza wananchi wa mkoa wa Dodoma kwa kuchangia nguvu zao kwenye ujenzi wa shule mpya 50 za sekondari.
 
Rais Kikwete alitoa pongezi hizo juzi usiku, kwenye sherehe fupi ya kuhitimisha michango ya elimu, kuchangia ujenzi wa shule za sekondari mkoani Dodoma, iliyofanyika kwenye ukumbi ulioko viwanja vya Bunge.
 
Mkoa wa Dodoma umekusanya fedha taslimu sh. 638,511,728 kutoka kwa wananchi wa mkoa huo, ambapo kima cha chini cha mchango kilikuwa sh. 5,000.
 
“Nimehamasika kwa utaratibu huu wa kuchangia kwa lengo la kuendeleza watoto kupata elimu, hii imethibitisha kuwa inawezekana kabisa watu kujitafutia maendeleo wenyewe, bila msaada… inawezekana popote nchini,” alisema Rais Kikwete.
 
Alikumbusha kuwa ni jambo la aibu kwa binadamu kuombaomba kila wakati au kumsubiri mfadhili katika jambo ambalo linawezekana dhahiri kujisaidia wenyewe.
 
“Kuchangia sh. 5,000 ni sawa na kuku wawili na inawezekana lakini bila ya moyo wa kuchangia siku zote utatangaza umasikini wako,” alisema.
 
Alisema serikali itahakikisha kuwa shule hizo mpya zitakaguliwa na kusajiliwa hivyo kupokea wanafunzi wote wa sekondari tayari kwa masomo kuanzia Januari, mwakani.
 
Awali akitoa maelezo ya michango hiyo ya elimu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, William Lukuvi alisema wanafunzi 24,078 kati ya 28,679 wamefaulu mtihani wa darasa la
 
Saba (asilimia 83.95) ya watahiniwa woteikilinganishwa na asilimia 77.79 mwaka jana.
 
Alisema mkoa umeweza kuchagua wanafunzi 11,315 (asilimia 47) tu ya waliofaulu kwa kutumia shule za zamani, wakati waliobaki 12,763 (asilimia 53) watachaguliwa katika shule mpya ambazo wanaziombea usajili mwezi huu, na nyingine Machi, mwakani.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.