Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  TUCTA yapinga makato mishahara ya wafanyakazi
TUCTA yapinga makato mishahara ya wafanyakazi
By Habari Tanzania | Published  12/21/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Tiganya Vincent, MAELEZO- Tanga
 
SHIRIKISHO la Vyama Huru vya Wafanyakazi (TUCTA) mkoani hapa, limekataa wafanyakazi wa wilaya ya Tanga, kukatwa asilimia 10 ya mishahara yao kuchangia kinachodaiwa miradi ya halmashauri ya jiji la Tanga.
 
Kauli ya kukataa makato hayo ilitolewa jana na Mratibu wa TUCTA mkoa, Innocent Allute, wakati akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo, Fortunatus Fwema msimamo huo wa shirikisho hilo.
 
Mratibu huyo alimweleza Kaimu Mkurugenzi huyo kwamba kikao cha TUCTA cha Desemba 15, mwaka huu kilitafakari kwa kina suala la makato ya asilimia 10 ya mshahara wa mfayakazi kwa maelezo ya kuchangia elimu.
 
Alisema viongozi wa vyama vya wafanyakazi
 
wanaujua umuhimu wa elimu na wanakiri kwamba wilaya ipo nyuma katika maendeleo ya sekta hiyo, lakini wanatofautiana na halmashauri ya jiji kuamua kuwakata kiwango hicho watumishi bila ya
 
kuwashirikisha na kuwahamasisha kushiriki katika mpango huo.
 
Allute ambaye pia ni Katibu wa TUICO mkoani hapa, alisema TUCTA haikubaliani na suala la kuwakata mishahara wafanyakazi bila ya ridhaa yao na wanaitaka halmashauri hiyo iwaite watumishi wote na kuwahamasisha wakubali kuchangia kwa hiari yao na si vinginevyo.
 
Alisema siyo utaratibu wa sheria za kazi, mwajiri kukata mshahara wa mfanyakazi bila ya makubaliano na mfanyakazi mwenyewe.
 
Akizungumza baada ya kikao hicho, Fwema alisema michango hiyo ni kwa ajili ya kufidia ujenzi wa vyumba 44 vya madarasa ambavyo vitagharimu sh. milioni 400.
 
Fwema alikiri kupokea barua inayoonyesha tamko la TUCTA ikipinga mpango unaotumiwa na halmashauri
 
kuwakata asilimia 10 ya mishahara yao watumishi wote wilayani humo.
 
Alisema wameandaa utaratibu wa kukutana na wafanyakazi kuwaeleza nia na madhumuni ya uamuzi huo ambao umelenga kukabiliana na upungufu wa madarasa, ili kuweza kuwapatia nafasi za kuendelea na masomo wanafunzi waliokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.