Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  JK akerwa mahindi kuanikwa chini
JK akerwa mahindi kuanikwa chini
By Habari Tanzania | Published  06/12/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Rais Jakaya Kikwete, ametoa siku saba kuanzia jana kwa uongozi wa soko la kimataifa la mahindi la Kibaigwa kurekebisha tabia ya kuanika mahindi katika mazingira machafu.

Rais Kikwete alitoa agizo hilo jana baada ya kutembelea soko la kimataifa la Kibaigwa na kujionea jinsi mahindi yalivyoanikwa katika mazingira machafu huku wananchi wakiyakanyaga.

Akiwahutubia wananchi katika soko hilo, Rais Kikwete alisema amesikitishwa kuona chakula kinacholiwa na binadamu kinaanikwa katika hali ya uchafu namna ile.

’’Kwa kweli nimesikitishwa na kitendo cha uongozi wa soko kuanika mahindi katika mazingira machafu namna hii, chakula wanachokula binadamu hakiwezi kuanikwa namna hii’’ alisema.

Aliongeza ’’mnayaanika kwenye uchafu, mnaweka kwenye magunia na mnakwenda kuwauzia wananchi, hii tabia yenu mbaya,’’ alisisitiza.

Alitaka apewe taarifa za kujirekebisha tabia hiyo katika kipindi cha wiki moja na kumwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. William Lukuvi, kufuatilia agizo hilo mara moja.

Na katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliwaasa wakazi wa Kibaigwa na Chalinze kutunza vizuri chakula watakachovuna katika msimu huu ili kuhakikisha kuwa hawapati tena tatizo la njaa.

Hata hivyo, aliwakumbusha wananchi hao kuwa, mwanzo na mwisho wa msimu wa kilimo ndiyo mwanzo wa maandalizi ya msimu ujao ambapo aliwataka watilie maanani katika kilimo cha mtama na uwele.

Alisema serikali itajitahidi kutafuta mbegu za mtama na uwele wa kutosha kwa ajili ya kusambaza kwa wananchi lakini akawaonya kuwa hawatapewa mbegu za mahindi bali watakaotaka kulima mahindi watafute mbegu wenyewe.

Ziara ya Rais Kikwete pamoja na mambo mengine, ilikuwa na lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumchagua katika wadhifa huo na CCM kuongoza dola katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.