Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Walioua polisi, mhasibu Vingunguti wakamatwa
Walioua polisi, mhasibu Vingunguti wakamatwa
By Habari Tanzania | Published  12/19/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Irene Mark

WATUHUMIWA wanne wanaodaiwa kuhusika kwenye mauaji ya askari polisi na mhasibu wa Kampuni ya Mohamed Enterprises (METL), Jumamosi iliyopita, wamekamatwa kwenye mahakama hiyo.

Watuhumiwa hao walikamatwa saa tatu asubuhi na askari polisi aliyejulikana kwa jina moja la Christopher, walipofika mahakamani hapo kusikiliza kesi ya kukutwa na silaha isivyo halali inayowakabili.

Waliokamatwa mahakamani hapo ni Ramadhan Mbano (30), Joseph Lyamuya (45), Selemani Yona (53) na Abdallah Said (49). Kesi hiyo namba 202/2006, ipo mbele ya Hakimu Mkazi, Elizabeth Mkwizu.

Inadaiwa kwamba katika kesi hiyo watuhumiwa hao walikutwa na bastola namba 87894, revolver na riffle namba 54C17999, zilizokuwa na risasi 23, kinyume cha sheria.

Ijumaa iliyopita, watuhumiwa hao hao waliachiwa huru katika kesi ya mauaji ya watu wawili iliyokuwa ikiwakabili baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kusema kwamba hawana kesi ya kujibu katika shitaka hilo la mauaji.

Awali watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Septemba 22 mwaka huu kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili eneo la Buguruni, Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Abdalla Mssika, aliwataja watuhumiwa wengine watatu waliokamatwa juzi kutokana na tukio hilo kuwa ni Aboubakar Hamisi (29), Omary Shauri (36) na Omary Mohamed (36).

Polisi inaendelea kumshikilia dereva wa gari la Kampuni ya MeTL, Juma Saidi, kutokana na tukio hilo. Aidha, Kamanda Mssika, alisema polisi inaendelea na uchunguzi zaidi ili kuwakamata wote wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita saa nne asubuhi kwenye njia panda ya Bombom, eneo la Vingunguti, jijini Dar es Salaam, ambapo watu wanne wanaodhaniwa kuwa majambazi walipora zaidi ya sh milioni 48, mali ya MeTL.

Waliouawa katika tukio hilo ni askari polisi F7091, PC Godwin Mkumbo na Mhasibu wa kampuni hiyo, Alsghar Sajjad.

Wakati huo huo, upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile-Mzuzuri, bado haujakamilika, hivyo kumfanya kuendelea kubaki rumande.

Akiomba kuahirishwa kwa kesi hiyo jana, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Charles Kenyella, alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi, Michael Luguru, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba tarehe ya kutajwa tena kwa kesi hiyo.

Kabla ya kuahirisha kesi hiyo, Wakili wa utetezi Dk. Ringo Tenga, alisisitiza kuharakishwa kwa upelelezi wa kesi ili mteja wao aweze kuomba dhamana Mahakama Kuu.

Mbali na maombi ya uharakishwaji wa upelelezi, wakili Tenga, alimpongeza Mwendesha Mashitaka wa kesi hiyo, Charles Kenyella, kwa kupanda cheo. Kenyella, alikuwa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), sasa amekuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP).

“Kupanda cheo kwa mwendesha mashitaka, kunaonyesha jinsi alivyo mchapakazi…ni imani yetu kwamba upelelezi wa kesi hii utaharakishwa…napenda kumpongeza,” alisema Tenga.

Baada ya maelezo na pongezi za wakili Tenga, Hakimu Luguru, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 2, mwakani itakapotajwa tena, kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika.

Mtuhumiwa huyo anatetewa na jopo la mawakili linaloongozwa na wakili wa kimataifa Nimrod Mkono, ambaye jana hakuwapo mahakamani hapo, na badala yake aliwakilishwa na wakili Joan Mwaikyusa.

Mawakili wengine wanaomtetea Ditopile ni Cuthbert na Dk. Tenga.

Ilidaiwa mahakamani hapo kwamba, Novemba 4 mwaka huu saa moja usiku, kwenye makutano ya barabara za Bagamoyo na Kawe, Ditopile, alimuua dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), kwa kumpiga risasi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.