Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mzazi kuishitaki Wizara ya Elimu
Mzazi kuishitaki Wizara ya Elimu
By Habari Tanzania | Published  12/19/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Anthony Kayanda, Kigoma

MKAZI wa jijini Dar es Salaam, Daruweshi Salum, ametishia kuipeleka mahakamani, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, akidai kupotelewa na mwanawe aliyekuwa akisoma kwenye Shule ya Sekondari Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Daruweshi, alisema kuwa, mtoto wake aitwaye Shaibu Daruweshi, mwanafunzi wa kidato cha sita kwenye shule hiyo, alifukuzwa shuleni kuanzia Novemba 5, mwaka huu, lakini hajaonekana nyumbani kwao tangu kipindi hicho.

Daruweshi alisema amelazimika kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma ili kujua nini kimemkwaza mtoto wake na kushindwa kufika nyumbani.

Alisema alipofika Kigoma, alimuona kaimu mkuu wa shule, na akamweleza kuwa, mtoto wake alipoondoka shuleni hapo, alichukua vitu vyake vyote akielekea nyumbani kwao Dar es Salaam.

Baada ya hapo, Daruweshi alikwenda kwenye kituo cha Polisi cha Kati mjini hapa na alipowaeleza askari, walimshauri akaonane na Mshauri wa Elimu Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma, Patrice Wangilisasi.

Mshauri huyo alimwagiza aende kwa Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Azim Premji, ambaye alimwambia kuwa jukumu la mwanafunzi kwenda nyumbani ni la mzazi mwenyewe na shule haihusiki na upotevu wa mtoto huyo.

Lakini Daruweshi alipingana na maelezo ya Premji akisema kuwa, ni jukumu la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na shule hiyo kumtafuta mtoto wake.

“Ni jukumu la shule kumfikisha mwanafunzi nyumbani kwa wazazi wake na kumkabidhi, wanapomfukuza,” alisema mzazi huyo.

Alisema kuwa, endapo mtoto wake hataonekana mahala popote mpaka mwishoni mwa mwezi huu, atalazimika kuifungulia wizara hiyo kesi mahakamani.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu kutoka Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Azim Premji, alisema ni kweli bodi hiyo iliwafukuza wanafunzi 14, Novemba 5, mwaka huu kwa utovu wa nidhamu.

Premji alisema wanafunzi hao walishiriki kuwapiga na kuwajeruhi walimu na kushawishi wanafunzi wengine kugoma kula chakula.

Alisema kwamba, mwanafunzi huhesabiwa kama mtoto akiwa shuleni, lakini anapovuka mipaka ya shule, huchukuliwa kama mtu mzima, hivyo jukumu la shule si kuwasafirisha wanafunzi wanaofukuzwa shule, bali ni la mzazi mwenyewe.

Premji alisema kuwa, mwanafunzi huyo alitoa anuani ya uongo alipokuwa shuleni hapo, na mzazi wake alipofika, alitoa anuani nyingine.



How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.