Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  ‘’Endelezeni uzalendo hata mkiwa nchi za nje’’- Balozi Maajar
‘’Endelezeni uzalendo hata mkiwa nchi za nje’’- Balozi Maajar
By Habari Tanzania | Published  12/17/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mwandishi wa HabariTanzania.com, London

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Bi Mwanaidi Sinare Maajar amewataka watanzania waliopo nchini hapa kuendeleza mapenzi kwa nchi yao bila kujali wapo ughaibuni ili kuweza kuendeleza taifa lao.Balozi Maajar aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na watanzania katika mkutano wa kwanza baina ya watanzania na Ubalozi wa Tanzania nchini hapa.

Balozi Maajar aliwaasa watanzania hao kuachana na fikra potofu kwamba ni serikali au ubalozi unaoweza kuwaletea maendeleo, ‘’kinachofanyika ni kwa serikali kujenga mazingira na wananchi kutumia fursa zinazotolewa, hivyo basi ni vyema mkafuata ule msemo maarufu wa Rais wa zamani wa Marekani aliesema usijiulize nchi yako imekufanyia nini bali ni nini unaweza kuifanyia nchi yako’’ alisema Balozi Maajar katika hotuba yake ambayo mara kwa mara ilikatizwa kwa makofi.

Aidha akizungumzia malengo hasa ya mkutano huo Balozi Maajar alisema anadhani wakati umefika sasa kwa Watanzania nchini Uingereza kuweza kuwa na umoja wao ambao utawawezesha Watanzania waliopo nchini hapa kuwa pamoja na kupata jukwaa la kutoa na kubadilishana mawazo juu ya yanayoendelea nchini Tanzania na namna wanavyoweza kushiriki.

‘’Umoja ambao ningewashauri muuanzishe utawawezesha ninyi kuwa na fursa ya kudhihirisha utaifa wenu hasa kwa wale ambao mmekuwa nchini hapa kwa muda mrefu na hivyo mtaweza kuwaonyesha watoto wenu utanzania wenu na kuwajenga kizalendo tangu wakiwa wadogo’’ alisema Balozi Maajar.

Mkutano huo uliohudhuriwa pia na maofisa wa Ubalozi akiwemo Mkuu wa Utawala, Bi Radhia Msuya, Mwanasheria wa ubalozi huo, Bi Carolyne Katana, Mwambata wa Ulinzi, Brigedia Jenerali Mwanga, Mkuu wa kitengo cha Uhamiaji, Bwana Sylvester Ambokile, Mkuu wa kitengo cha Fedha, David Nginia, Afisa Utawala,Bwana Kiondo, Mwambata wa Masuala ya Habari na Mawasiliano, Bwana Iddrisa Zaharani.

Katika mkutano huo, Balozi alipendekeza kuundwe kamati ya muda ya viongozi wa jumuiya ya watanzania nchini Uingereza ambayo itapewa jukumu la kutengeneza katiba na kuitisha uchaguzi mkuu wa kuanzisha rasmi jumuiya ya watanzania waishio Uingereza.

Kamati iliyoundwa ina wajumbe kumi ambao ni mwanahabari wa siku nyingi, Juma Pinto, Afisa wa Benki ya New York nchini hapa, Norah Sumari, Mwanasheria Antony Huka, Aliekuwa rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha IFM Tanzania alieko masomoni Bwana Omari Lambi, Bi Rehan Said Olofi kutoka Zanzibar, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake nchini hapa, Bi Mariam Kilumanga, Mtangazaji wa BBC, Saidi Yakubu, Mmoja wa waanzilishi wa taasisi ya zamani ya Watanzania Bi Lucy Shigikile, na Bwana Hassan Hafidh.




How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Kirongozi Breen)
    Rating

    The Tanzania Ambassador to the UK. Has the best i dear and she is a considerate person, as she is treating her national citizens as like her own kids it is very rare to see a high ranked person to think about regular citizens.Especially for Tanzanian leaders.I do appreciate hon Maajar for her kindness.she brought lot of hope to our Tanzanians who live overseas in general.
     
Submit Comment


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.