Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Kutoka kwa Wasomaji  »  Mh.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Mh.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
By Nestory K. Manoni | Published  12/16/2006 | Kutoka kwa Wasomaji | Rating:
Na HabariTanzania.com

Napenda kuwapongeza vijana wote waliochaguliwa kama washindi baada ya Mtihani wa Darasa la Saba.
Kinachonisikitisha na kunikatisha tamaa kama mmoja wa wazazi nipale ambapo suala la baadhi ya wasimamizi kuendeleza wimbi la kutoa mitihani kwa baadhi ya wanafunzi kinyume cha utaratibu.

Kitendo hiki pia kinavunja moyo na kuwanyima haki wanafunzi wanaotumia uwezo wao kiakili kutaka kushinda mitihani hiyo lakini wanashindwa kufikia malengo hasa watoto wa masikini kwa kuwa wanaoonekana kushinda ni wale wanaofanyiwa mpango wakati wa mitihani hiyo.

Lakini kwa hali halisi wengi wao hawana uwezo wa kumudu mitihani hiyo iwapo mbinu hizo zisipotumika na ukiwafuatilia sana hao wanaoshinda mitihani kwa asilimia ya juu sana wanapata alama za mwisho kabisa wanapofikia mtihani wa mwisho wa kumaliza elimu ya sekondari.

Suala la baadhi ya shule kugundulika na nyingine kutogundulika ni jinsi gani umahili wa kufanikisha mipango hiyo ulivyofanyika,pengine wazoefu wame-adivance zaidi mbinu hizo au waliogundulika waliishi kwa mazoea yale yale na mbinu zile zile, hili ni tatizo la nchi nzima.

Je,udanganyifu huu utaendelea hadi lini ili na wale wasiokuwa na uwezo wa kudanganya wapate haki zao za kimsingi katika elimu?

Inasikitisha sana kuona kuwa wanafunzi wanafutiwa mitihani na hivyo kutohesabika kabisa kuwa walihitimu elimu ya msingi katika nchi yao kwa manufaa ya watu wachache tu.

Ni vema serikali ikatazama na kuamua adhabu nyingine kwa wahusika kuliko kuwaadhibu hao wanafunzi kiasi hicho, ikizingatiwa kuwa wengi wao ni watoto waliochini ya umri wa miaka 16,hivyo kisheria hawana kosa la moja kwa moja kuweza kuwatia hatiani.

Kama watoto akili yao haiwezi kwa urahisi kupinga maamuzi yaliyofikiwa na wazazi wao na walimu wao katika harakati za kuandaa mipango hiyo,na kama wanaonekana kuwa na kosa la moja kwa moja ni vema wakashitakiwa kama waharifu ili uchunguzi wa kisheria ukafanyika kuliko kuwahukumu kijumla jumla.

Kufanikiwa kwa udanganyifu huo ni rushwa,kwa kuwa sheria ya kosa la kutoa na kupokea rushwa ipo na adhamu inajulikana kupitia mahakama ni bora zaidi ikatumika kuliko hiyo ya kufuta matokeo kwa shule nzima wakiwemo hao walemavu waliotajwa,nani ataubeba huo mzigo mzito iwapo serikali inawazuia kujiendeleza ki-elimu?

Adhabu ya kufuta matokea mashuleni imedumu kwa muda wa miaka mingi sana hapa nchini,hivi sheria hiyo inayonyima haki za watoto kielimu haiwezi kuboreshwa kiasi kwamba watoto wa shule wasihusike moja kwa moja katika uhalifu huo kwa kuwa katika harakati za kuandaa mpango wa kuonyesha mitihani watoto wanaohusika hawashirikishwi moja kwa moja ila hupokea maelekezo kutoka kwa walimu na wazazi wao kwa kushirikiana na wasimamizi wa mitihani.

Natambua bayana jitihada za awamu ya nne kuwa haitaki kuendeleza uharifu uliokithiri hapa nchini kwa baadhi ya watendaji wa umma lakini pamoja na mazuri hayo ni bora suala la wanafunzi kuonyeshwa mitihani kinyume cha utaratibu liangaliwe kwa makini na kuamuliwa kwa manufaa ya jamii nzima ya watanzania ili kuwanusuru watoto ambao ni hazina kubwa ya taifa katika mambo mbalimbali ya kuijenga na kuiendeleza nchi.

Dereva anayekwepa kumgonga msafiri mmoja barabarani na kusababisha kuiingiza mtaroni gari iliyobeba abiria 60 au zaidi na kusababisha vifo vya watu wengi,huyo si dereva makini na hafai kabisa kuendelea kuendesha.
Si vizuri sheria inayotumika sasa kuadhibu watoto inayofanana kabisa na mfano huo ikaendelea kutumika kwa manufaa ya wachache.

Nakupongeza sana Mh.waziri mama Sitta kwa kutotaja shule zilizoshinda,haina maana kuendelea na mfumo huo maana unachochea kwa kiwango kikubwa sana mazingira ya rushwa kwa kuwapa wasimamizi chochote watakacho ili watoto wa shule husika wapewe mitihani kinyume cha utaratibu kama sehemu ya kutangaza sifa ya jina la shule (promotion)ili mwaka unaofuata wazazi wajikaange kwa mafuta yao kupeleka watoto wengi zaidi katika shule hiyo hasa shule za baadhi ya wamiliki binafsi,kwa kuwa mfumo mkuu wa shule hizo imekuwa ni biashara tupu na si vinginevyo.

Utashangaa kuona kuwa shule za serikali tuition na pre-form one vimepigwa marufuku lakini katika shule za watu binafsi ambako ada ni kubwa sana bila udhibiti wowote,tuition, pre-form one,ununuzi wa ream za karatasi A4 na kuchangia majengo ndo vimepamba moto.

Kivutio kimekuwa ni kuongea Kiingereza,Kifaransa na kujifunza computer tu na kwa kuwa wazazi wengi hatujui Kiingereza wala computer,tunafarijika kuweka watoto katika shule hizo kwa nia njema kabisa,lakini mwisho wa siku hakuna kinachoonekana.

Mfano mzuri ni pale baadhi ya shule hizo zinapogundulika kuhusika na mchezo huo mbaya wakati zinawatoza wazazi fedha nyingi za ada ili watoto wao wawe na uwezo mzuri wa kushinda masomo bila mizengwe.

Mh.mama Sitta umefika wakati muafaka wa kuzifanyia kazi shule hizo ili ziendane na malengo yake na siyo kuendelea kuwaibia wananchi kwa janja ya nyani.

Kwa kuwa serikali haina uchoyo wa kuwabagua wanafunzi wanaofaulu kutoka shule za wamiliki binafsi kwa kutoa nafasi za kuendelea na masomo popote nchini, ni vema nao wakahusika kuondoa baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kuwa ni kero kubwa kwa wazazi kama vile ada za tuition, michango ya majengo na ununuzi wa bunda zima la karatasi A4 kila mwaka Sheria ni msumeno.

Kwa upande wa shule za serikali,ni vema wizara husika ikapunguza vitisho vyake kwa wakuu wa shule na maafisa elimu kwa maeneo yanayoshindwa kufanya vizuri kwa kuboresha zaidi mazingira ya ufundishaji,kuweka walimu wa kutosha mashuleni na wenye sifa nzuri ,unategemea nini unapompangia mwalimu kufundisha masomo zaidi ya yale aliyojifunza chuoni kwenda kuyafundisha mashuleni,huo ujuzi wa masomo ya ziada kaupata wapi na hatimaye kuwezesha watoto washinde kwa alama za juu kuliko wale waliofundishwa na mwenye ujuzi kwa masomo husika? lazima atumie mbinu ili kutangaza jina lake na kuepuka vitisho iwapo mwanya unapatikana.

Motisha kwa walimu hasa wanapokwenda kusimamia mitihani,"Per diem" iwe nzuri ili kuwapunguzia vishawishi,lakini pia wapewe nafasi ndogo sana ya kukutana na wenyeji wao wanapokwenda kusimamia mitihani hiyo.

Mh.Waziri napenda kutoa ombi iwapo inawezekana watoto waliopatikana na makosa wasamehewe na kuruhusiwa kurudia mtihani chini ya usimamizi mzuri na waliohusika kufanikisha uhalifu huo wachukuliwe hatua za kisheria iwe mfano kwa wengine wenye tabia kama hizo kwa kukwamisha maendeleo ya taifa.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Nestory K.Manoni - neskitman@yahoo.com


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.