Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Lowassa ’awakwida’ trafiki
Lowassa ’awakwida’ trafiki
By Habari Tanzania | Published  06/11/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, amevikemea vikali vyombo vya dola vinavyosimamia usalama barabarani na kuvitaka viwe makini kuhakikisha ajali zisizo za lazima hazitokei kama ile ya basi lililoua abiria 54 na kujeruhi 20 mkoani Arusha juzi.

Ajali hiyo ililihusu gari aina ya Toyota DCM lenye namba za usajili TZH 1025 lililokuwa linatoka Mererani kuelekea mjini Arusha baada ya kugonga nguzo ya daraja na kutumbukia katika mto Malala wilayani Arumeru.

Bw. Lowassa aliyasema hayo jana wakati alipowatembelea majeruhi wa ajali hiyo katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru, hospitali ya wilaya Arumeru na eneo la tukio ambako gari hilo liliangukia kwenye mto huo.

Alisema ni vema wananchi wenyewe wawe makini na kuacha kupanda gari wanapoona limejaa na akawataka abiria kuwa wakali, pindi dereva anapoendesha gari kwa mwendo wa kasi.

Waziri Lowassa, aliwataka abiria kabla ya kuingia ndani ya chombo cha usafiri wahakikishe gari limebeba abiria kwa idadi inayotakiwa na sio vinginevyo.

Alisema basi lililopinduka lilitakiwa kubeba abiria 26, lakini kwa tamaa za kupata pesa nyingi lilibeba abiria 74 hali iliyosababisha kutokea kwa ajali hiyo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya mkoa Mount Meru, Dk. Naftari King’ori aliwataja majeruhi saba waliolazwa hospitali ya wilaya ya Arumeru kuwa ni Lilian Yohana (14), Happy Lucas (20), Elieshi Gabriel (45), Happy Wilson (10), Moses Godfrey (40), Goodluck John (32) na Laurence Robert (30).

Alisema hadi sasa miili ya marehemu 48 wa ajali wametambuliwa lakini maiti wawili hawatajambulia na kwamba wananchi bado wanaendelea kufurika kwenye hospitali hiyo ya mkoa ili kuwatambua.

Dk. King’ori aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Kuikoi Efrem, Mary Emmanuel, Neema Emanuel, Hamisi Mustafa, Hellen Charles, Monica Losium, Anna Gidion, Elius Solomon, Makete, Rahel Obed, Daniel Stephano, Raphael Mbise, Haji Seleman, Abdul Mohamedy na Patrice aliyetambulika kwa jina moja tu.

Wengine ni Eliamani Isaya, Regna Monoy, Maiko Olengatnyi, Beatrice Alibork, Mama Braity, Ester Augustino,Mwalimu L.O.Ayo,Batazari Elbeth,Elfraim Riukai, Mrs Emanuel Sikoyo, Winnfrida Piniel, Happy Kevii, Juliane Amani, Simon John, Juma Ramadhani na Tareto Kiseto.

Marehemu wengine ni Miraja Rashidi, Livingstony Martin, Juma Lelo, Lilian Elius Asha Msomali, Edward Kirenga, Joseph Joshua, Masa Wenge, Kezia Shami, Martha Naomi, Maua Rajabu, Halima Sefu, Max Silayo na Joshua Silayo, Witness Winece na Unice Winese.

Dk. King’ori alisema majeruhi watatu kati ya majeruhi wote 20 wa ajali hiyo wameruhusiwa na majeruhi 17 wamebaki katika hospitali ya mkoa na saba wako hospitali ya wilaya Arumeru.

Ajali hiyo mbaya kuliko zote nchini kwa mwaka huu, ilitokea juzi majira ya saa 7.00 mchana huko wilayani Arumeru, baada ya basi hilo kuangukia kwenye mto Malala ulioko wilayani humo.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.