Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mulamula Katibu Mtendaji Maziwa Makuu
Mulamula Katibu Mtendaji Maziwa Makuu
By Habari Tanzania | Published  12/16/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Maura Mwingira

RAIS Jakaya Kikwete amemteua Balozi Liberata Mulamula, kuwa Katibu Mtendaji wa kwanza, kuongoza Sekretarieti ya Ukanda wa Maziwa Makuu.

Taarifa ya Ikulu jana inaeleza kuwa, Mulamula ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo na utadumu kwa miaka minne.

Rais Kikwete alisema kuwa Tanzania imepewa nafasi ya kutoa Katibu Mtendaji, na kwa sababu uteuzi huo ni wa haraka, amemteua mwanadiplomasia huyo mwenye uzoefu wa muda mrefu.

Mara baada ya taarifa hiyo, ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe na vigelegele, hali iliyodhihirisha kukubalika kwa uteuzi wa Rais Kikwete.

“Shangwe hii inadhihirisha kukubalika kwa mteule wetu,”alisema Rais Kikwete, hali iliyoamsha shangwe kutoka kwa wajumbe wa mkutano.

Mara baada ya uteuzi huo, Balozi Mulamula aliahidi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, na kushirikiana kwa karibu na viongozi wakuu wa nchi hizo, ili kuhakikisha kwamba amani, utulivu na maendeleo yanatawala katika eneo hilo.

Kabla ya uteuzi huo, Balozi Mulamula alikuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Katika mkutano huo, Rais Kikwete alisema kuwa Tanzania inaahidi kutoa dola za Marekani 259,366 kusaidia sekretarieti ya ukanda huo na dola 500,000 kwa ajili ya mfuko maalumu wa ustawishaji na maendeleo.

Ofisi za Sekretariati ya Ukanda wa Maziwa Makuu itakuwa Bujumbura, Burundi


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.