Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Sekta ya afya waombwa kuendelezwa
Sekta ya afya waombwa kuendelezwa
By Habari Tanzania | Published  12/15/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imeombwa kuwaondelea kielimu watumishi wake mkoani Ruvuma.

Ombi hilo limetolewa na watumishi hao wakati wakizungumza na Mwananchi kuhusiana na vikwazo wanavyokumbana navyo katika utekelezaji wa kazi zao kutokana na kukosa ujuzi wa kutumia vifaa vya kisasa.

Mmoja wa wafanyakazi hao ambaye ni Fundi Msanifu Msaidizi Kitengo cha X-ray na Ultrasound, Moza Chita alisema watumishi wengi wa sekta hiyo wanahitaji kujiendeleza hasa katika kipindi hiki cha matumizi ya teknolojia za kisasa.

Chita alitoa mfano wa vifaa vya kisasa vikiwamo vya maabara ambavyo wamekuwa wakipelekewa kuwa imekuwa ni vigumu kwao kuvitumia kutokana na kuhitaji ujuzi zaidi.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma , Dk Luitfrid Komba ameiomba serikali kuwaendeleza watumishi hao ili waweze kuisaidia jamii kuboresha afya za watanzania.

“Watumishi wengi wanahitaji elimu na wameonyesha nia ya kujiendeleza kimasomo, lakini wanakwamishwa na hali ngumu ya maisha kwani maslahi yao ni duni na haya watoshelezi kuendesha maisha yao,” alisema Dk Komba

Awali, watumishi hao, waliitaka serikali kuiangalia upya sekta hiyo ya afya kwa kuwaongezea maslahi na kuwalipa malipo ya ziada na dharura.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.