Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Moto wateketeza Soko la Mwanjelwa
Moto wateketeza Soko la Mwanjelwa
By Habari Tanzania | Published  12/14/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Brandy Nelson, Mbeya

SOKO Kuu la Mwanjelwa jijini hapa, limeteketea kwa moto na kusababisha vilio, simanzi na watu 20 kujeruhiwa, baadhi yao kupoteza fahamu baada ya mali zao za mamilioni ya fedha kuharibiwa.

Moto huo ulitekeza zaidi ya vibanda 506 na mali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi, ambazo thamani yake halisi bado haijafahamika.

Soko hilo lilikuwa linategemewa na wakazi wengi wa Mkoa wa Mbeya na nchi jirani za Zambia na Malawi ambao walikuwa wakitumia soko hilo kwa mahitaji ya vyakula, mavazi na mahitaji mengine muhimu.

Kutokana na moto huo, ulioanza majira ya saa 1.00 jioni na kuwashinda zimamoto, baadhi ya wafanyabiashara walipoteza fahamu na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, huku wengine wakiangua kilio kutokana na kupoteza mali na fedha, na wengi walisikika wakisema kuwa ndani ya maduka yao kuna mamilioni ya fedha.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia kikosi cha zimamoto cha Halmashauri ya Jiji kikishindwa kuuzima moto huo kwa madai kuwa baadhi ya mabomba ya kutolea maji yaliyopo jirani na soko hilo kuziba.

Mbali na magari mawili ya kikosi cha kuzima moto ya Halmashauri ya Jiji, pia lilikuwepo gari dogo la kikosi cha kuzima moto la Uwaja wa Ndege lenye namba SM 4633, lakini yote hayakufua dafu na moto huo ulioendelea kuteketeza soko hilo.

Vibaka walionekana wakibomoa baadhi ya maduka bila wenyewe kuwapo na kujifanya kama wanaokoa mali kumbe walikuwa wakiziiba.

Hali ya utulivu ilirejea baadaye baada ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kumwagwa katika eneo hilo na kuanza kutembeza kipigo bila kujali kama ni wamiliki wa maduka au askari polisi waliovaa nguo za kiraia.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia polisi mmoja wa kike ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, akipata kipigo kutoka kwa askari wa JKT ambao walikuwa wakiwatanya watu waliokuwa karibu na maduka.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Suleiman Kova, alisema taarifa za awali zinaeleza kuwa moto huo ulianzia kwa fundi cherehani aliyejulikana kwa jina la Sikujua Mkulima.

Alisema kuwa chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme, akisema kutokana na kukatika mara kwa mara kwa umeme kulisababisha kuzuka kwa moto ambao wananchi walishindwa kuuzima.

Alisema gari la zimamoto liliwahi kufika eneo la tukio, lakini lilishindwa kutoa msaada wowote kutokana na miundo mbinu mibovu ya soko hilo iliyolizuia magari kuingia ndani na kuzima moto.

Mbali ya miundombinu mibovu, Kova alisema sababu nyingine za kushindwa kuzimwa moto huo ni visima vilivyopo katika soko hilo kutofanya kazi pamoja na ujenzi mbaya wa soko, maduka mengi yakiwa yamejengwa kwa mbao.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa, Dk. Eliuter Samky, alisema usiku wa kuamkia jana, walipokea majeruhi 20 na kwamba majeruhi wawili walitibiwa na kurusiwa.

Hadi majira ya saa 4.00 asubuhi jana,moto huo ulikuwa ukiendelea kuwaka katika maeneo ya katikati ya soko hilo, na gari la zimamoto kutoka Mkoa wa Iringa liliwasili mkoani hapa majira ya asubuhi kuja kusaidia kuzima moto huo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Njimba)
    Rating
    Ninawapa pole wote wliopotewa na mali zao. Lakini hili liwe fundisho ili hali ya masoko yote nchini Tanzania iangaliwe. Na mamlaka zinazohusika majiji, manispaa, halmashauri ziangalie masoko yao kam yako tayari kwa ajali kama hizi. Na mara kwa mara wawe wanaangalia kaa wako tayari. Badala ya kuangalia makusanyo ya kodi tu.
    Poleni sana wote mlio potelewa na mali zenu na mlio jeruhiwa.
    Njimba
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.