Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Pemba sasa kupata umeme gridi ya taifa
Pemba sasa kupata umeme gridi ya taifa
By Habari Tanzania | Published  12/12/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mwandishi Wetu

KISIWA cha Pemba kimo mbioni kuunganishwa na gridi ya taifa baada ya mkataba wa kutandaza nyaya chini ya bahari kutokea Tanga kusainiwa jana.

Utiaji saini wa mkataba huo uliwahusisha, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Khamis Mussa kwa upande wa Serikali ya Zanzibar (SMZ) na Mwakilishi wa Ubalozi wa Norway nchini, Kristine Sverdrup.

Chini ya mkataba huo, ambao hata hivyo hakuelezwa utaanza kutekelezwa lini, serikali ya Norway itatoa Sh54.3 bilioni kwa kazi ya kutandaza nyaya chini ya bahari kutoka Pangani, Tanga, hadi Wesha Chake Chake, Pemba, na kuwezesha kiwasiwa hicho kuungana na gridi ya taifa.

Mradi huo utawaondolea adha wananchi wa kisiwa cha Pemba ambao kwa muda mrefu walikuwa wakitumia umeme usio wa uhakika wa nguvu za mafuta, uliokuwa unaigharimu serikali Sh600 milioni kila mwezi kwa ajili ya kuendeshea vinu vinne vya kuzalisha umeme kisiwani humo.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini huo, Sverdrup alisema serikali yake imeridhishwa na utekelezaji wa juhudi za maendeleo ya kupambana na umasikini nchini na kuamua kusaidia maendeleo ya wananchi wa Unguja na Pemba.

“Tumeridhishwa na jinsi misaada yetu inavyotumika kama tulivyokusudia kwa ajili ya wananchi wa visiwa hivi, ikiwemo kupambana na umaskini,” alisema Sverdrup.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid, alisema hadi kufikia mwaka 2008 asilimia 82 wananchi wa Zanzibar watakuwa wamefaidika na umeme hadi vijijini.

Aliishukuru serikali ya Norway katika utekelezaji wake wa ahadi ambazo lengo lake kubwa ni kusaidia maendeleo ya wananchi wa Unguja na Pemba .

Serikali ya Norway imekuwa ikisaidia shughuli mbalimbali za maendeleo hapa Zanzibar, ikiwamo usambazaji umeme vijijini kwa awamu ya nne kuanzia awamu ya kwanza iliyoanza Oktoba 1986 na hadi Januari 1988.

Katika awamu hiyo, zilijengwa njia za umeme mkubwa zenye urefu wa kilomita 65 katika kisiwa cha Unguja na uwekaji wa transfoma 20 katika visima vya maji na zahanati, ambapo jumla ya Sh2,948,671,570 zilitumika


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.