Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mahakama yasitisha wamachinga kulipwa fidia
Mahakama yasitisha wamachinga kulipwa fidia
By Habari Tanzania | Published  12/12/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

NaTausi Ally

HAKIMU wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Bahati Ndeserua, amesitisha utekelezeji wa amri yake ya kuitaka Manispaa ya Ilala iwalipe wamachinga Sh70 milioni kama fidia ya hasara ya kuvunja vibanda vyao vya biashara.

Awali wamachinga hao wanaofanya biashara katika mitaa ya Nyamwezi na Nalung'ombe walifungua kesi mahakamani hapo wakitaka manispaa ya Ilala iwalipe fedha hizo kwa madai kuwa manispaa hiyo imevunja vibanda vyao huku kukiwa na amri ya mahakama inayozuia uvunjaji huo.

Wamachinga walishinda kesi hiyo na mahakama ya Ilala iliamuru manispaa ya Ilala iwalipe fidia ya Sh70 milioni. Hata hivyo, manispaa hiyo nayo iliwasilisha ombi katika mahakama hiyo, ikitaka mahakama hiyo isitishe amri hiyo hadi hapo kesi ya msingi kuhusiana na suala hilo itakapo malizika.

Baada ya Hakimu Ndeserua kupitia maelezo yaliyowasilishwa mahakamani hapo na wamachinga na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, John Lubuva, jana alisitisha uamuzi huo hadi hapo kesi ya msingi itakapokwisha.

Alisema ombi la Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala la kumtaka apitie upya uamuzi alioutoa wa kuwalipa fidia wamachinga hao atalisikiliza Januari 22.

Awali wakili Abubakar Salim anayewatetea wamachinga hao, alipinga kuahirishwa kwa kesi hiyo kwa madai kuwa hizo ni mbinu za kuchelewesha uendeshaji wa kesi wakati wateja wake hawana kazi yoyote na wanazidi kunyanyasika siku hadi siku.

Chama cha Jamii na Maendeleo ya Wamachinga wa jijini Dar es Salaam, kilifungua kesi dhidi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kikitaka kilipwe fidia kutoka na hatua ya manispaa yake kuvunja vibanda vyao


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.