Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ajali ya treni, radi yaua saba Singida, Mbeya
Ajali ya treni, radi yaua saba Singida, Mbeya
By Habari Tanzania | Published  12/10/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Waandishi Wetu

WATU saba wamekufa katika mikoa ya Singida na Mbeya kwa matukio ya ajali ya treni na radi zilizotokea katika maeneo hayo.

Kutoka Singida, Gasper Andrew anaripoti kuwa
watatu walikufa juzi baada ya mabehewa ya treni ya mizigo kuacha njia na kupinduka.

Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Celina Kaluba alisema watu hao walikufa Desemba 6 mwaka huu saa 5.30 usiku katika milimia ya Saranda wilayani Manyoni

Alisema treni ya mizigo Namba Y 22 yenye injini namba 8835 iliyokuwa ikiendeshwa na Jackson Njau(33), mkazi wa Kingurunyembe, Morogoro ilizidiwa na uzito wa mzigo wakati inateremka mlima huo. Treni hiyo ilikuwa na mabehewa 25 na kati ya hayo, mabehewa 19 yaliacha njia na kuanguka.

Alisema kati ya mabehewa hayo 19 yaliyopinduka, matatu yalikuwa yamebeba ng’ombe 120, mali ya mfanyabiashara wa mifugo Mwangeza Gwatebo, mkazi wa Urambo mkoani Tabora.

Kaluba alisema Robert Daud au Chongo (20), Advoness Utyatya(25) na Ngozi Sipoti(21), wote wakazi wa Urambo ambao walikuwa kwenye mabehewa yaliyobeba ng’ombe, walifariki dunia papo hapo baada ya kulaliwa na ng’ombe.

Alisema ng’ombe 40 nao walikufa papo hapo na wengine 15 waliibwa na watu wasiofahamika.

Kamanda Kaluba alisema dereva Njau alijeruhiwa vibaya kwenye korodani,kifuani na miguuni na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Alisema pamoja na Njau, watu wengine waliojeruhiwa ni, Said Ndeje(28), mkazi wa Morogoro, Stephen Ponera wa Dodoma, nao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni wakiwa na majeraha katika sehemu zao mbalimbali za miili yao.

Naye Mwandishi Wetu anaripoti kutoka Mbeya kuwa watu wanne wamekufa papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Suleiman Kova alisema kati ya hao waliokufa ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kimondo.

Kamanda huyo alisema watu walipigwa na radi wakati wakiwa wamejificha katika klabu ya pombe za kienyeji kusubiri mvua iishe.

Aliwataja wale waliokufa katika ajali hiyo kuwa Alex Adamu (15), ambaye ni mwanafunzi, Bahati Omary (25), Ernest Shungu (45) na Simon Jina (25), wote wakazi wa Kimondo, Wilaya ya Mbeya.

Aliwataja waliojeruhiwa vibaya katika ajali hiyo na kulazwa katika Hospitali ya Igogwe wilayani Rungwe kuwa ni Modesta Dona (25), Stephano Jonas(24), Richard Karonga(32) na Erasto Pombo(30).

Majeruhi wengine, aliwataja kuwa ni Tasio Modesta(30), Wilson Longopela(28), Robert Emmanueli(30), Omary Mwashipile (30) na Yohane Kinza (30), ambao wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 12:00 jioni na kwamba mwanafunzi huyo, Alex Adamu alikutwa na mauti hayo wakati akiwa amejificha katika klabu cha pombe za kienyeji wakati akisubiri mvua kubwa iliyokuwa inanyesha iishe na kwamba wengine watano walikuwa wakipata kinywaji klabuni hapo


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.