Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mkurugenzi mpya PCB kama Mwema
Mkurugenzi mpya PCB kama Mwema
By Habari Tanzania | Published  12/9/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

MKURUGENZI Mkuu mpya wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini (Takuru), Edward Hosea, ameanza kazi kwa kasi mpya baada ya kuamua kutangaza kwenye vyombo vya habari namba zake za simu na zile za watendaji wake.

Kiongozi wa kwanza kufanya hivyo, alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Said Mwema pindi alipoteuliwa na kuachana na ukiritimba uliokuwa unafanywa na aliyemtengulia, Omari Mahita.

Hatua ya Mwema kutoa namba yake ya simu na zile za wakuu wa polisi wa mikoa, imesaidia kupokea matukio mengi ya uhalifu moja kwa moja kutoka kwa wananchi.

Hosea, baada ya kuapishwa Jumatatu wiki hii, alilielezwa Mwananchi kuwa anakwenda kuanza kazi kwa ari, nguvu na kasi mpya na kwamba atadhihirisha mabadiliko ya utendaji wa Takuru katika miezi sita ijayo.

"Usiniulize kasi mpya sasa hivi. Njoo baada ya miezi sita uniulize kasi mpya niliyowaahidi. Kuapa sio ufumbuzi wa matatizo bali ni mwanzo wa safari," alisema Hosea wakati akijibu maswali ya mwandishi wa Mwananchi.

Namba yake ni 0754 763741, Naibu wake, Lilian Mashaka ni 0754 336116, Mkurugenzi Idara ya Utafiti, Udhibiti na Takwimu ni 0754 336060, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Upelelezi, Alex Mfungo ni 0784 998841 na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu kwa Umma, Mary Mosha ni 0784 998836. Namba za wakuu wa Takuru mikoa pia zinapatikana kwenye gazeti la jana.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, kuhusu uamuzi wa kutoa namba zake na wakuu wa Takuru wa mikoa, Hosea alisema katika uongozi ameamua kuwa muwazi na kuomba wananchi kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo.

"Kama hukutangaza simu hizo na kuonyesha uwazi huo, mwananchi wa kawaida sio rahisi kujua namba yangu ya simu na pindi anapopata taarifa za rushwa na kama akikwama sehemu zingine anaweza kuona ndio mwisho, nimeona ni bora tutoe namba za simu ili tuweze kufikika kwa urahisi," alisema Hosea.

Alisema hakuna siri kwenye taasisi hiyo ambazo zinaweza kuwafanya kuficha namba zao za simu na kwamba, iwapo wangeendelea kufanya hivyo wangekuwa wanajikwamisha wenyewe kiuntendaji.

Mkurugenzi huyo, ambaye kabla ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Takuru, alisema wananchi lazima wafahamu kuwa taasisi hiyo haina ubwana wala utwana, bali waliopo ni watumishi wao.



How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.