Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Maiti 25 wa ajali ya lori watambuliwa
Maiti 25 wa ajali ya lori watambuliwa
By Habari Tanzania | Published  06/9/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Wananchi Kibondo waomboleza
 
MAITI 25 kati ya 28 za watu waliofariki katika ajali ya lori juzi asubuhi mkoani Kagera zimetambuliwa na kuchukuliwa na jamaa zao.
 
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Ignas Mbinga alisema kuwa miili ya marehemu hao ilitambuliwa jana na maiti tatu bado hazijatambuliwa na zimehifadhiwa katika Hospitali teule ya Wilaya hiyo.
 
Mbinga alisema kuwa ajali hiyo ilitokea katika eneo la Lusahunga wilaya ya Biharamulo wakati lori namba T 655 AJQ lilipotaka kuingia barabara ya lami itokayo Isaka wilayani Kahama kwenda Rusumo, Ngara.
 
Dereva wa lori hilo Baraka Kafunga (34) alifikishwa mahakamani jana akishitakiwa kwa makosa 48 ya kusababisha vifo, mwendo wa kasi na kuendesha gari likiwa bovu. Alifikishwa mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Biharamulo na Hakimu Mrisho Kalibo na kusomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashitaka Alex Mkama.
 
Lori lililosababisha vifo hivyo lilikuwa limesheheni dagaa na abiria zaidi 50 na kwamba lilikuwa likitokea Biharamulo kwenda Kibondo mkoani Kigoma. Watu 28 walikufa papo hapo na wengine 15 walijeruhiwa na kulazwa.
 
Katika hatua nyingine, Serikali wilayani Kibondo jana ilitangaza kuwa siku ya maombolezo kufuatia vifo vya watu hao.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luteni Kanali John Mzurikwao alisema kutokana na uwingi wa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo, wilaya imelitambua tukio hilo kama maafa ya wilaya na kuwataka wakazi wote wa mji wa Kibondo na vitongoji vyake kuitambua siku ya jana kuwa ya maombolezo.
 
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo, Felix Kijiko ametuma salamu za rambirambi kwa wananchi wote wa wilaya ya Kibondo na ametoa wito kwa wananchi kuwa na mshikamano na kusaidiana katika kipindi hiki cha maombolezo.
 
Mmoja wa walionusurika aliyejitambulisha kwa jina la Anord mkazi wa kijiji cha Biturana wilayani Kibondo, amesema gari hilo aina ya lori tani saba walilokuwa wamepanda lilikuwa limesheheni magunia ya samaki pamoja na baadhi ya wafanyabiashara.
 
Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete ametuma salam za rambirambi kufuatia ajali ya lori iliyotokea juzi eneo la Lusahunga, mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 28 na wengine 13 kujeruhiwa.
 
Katika salamu zake hizo, alizozituma kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Enos Mfuru, Rais Kikwete, alisema: "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kusikitisha ya ajali mbaya ya gari iliyotokea leo (juzi) huko Lusahunga na kusababisha vifo vya Watanzania wenzetu 28 na wengine 13 kujeruhiwa."
 
"Ni wazi kuwa vifo hivyo vitakuwa vimeathiri maisha ya watu wengi. Watanzania hao waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni baba, mama, kaka na dada katika kaya fulani. Ni wazi kwamba vifo hivyo vitakuwa vimesababisha kuyumba kwa familia ambazo zimepoteza wapendwa wao," alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa vifo hivyo, si tu vimepoteza wakuu wa kaya, lakini pia vimepunguza nguvu kazi ya taifa.
 
Mbali na rambi rambi hizo, Rais Kikwete pia amewakumbusha madereva nchini kuwa makini na kuchukua tahadhari wanaposafirisha watu katika magari yao.
 
Kutoka gazeti la Uhuru
Na Angela Sebastian, Bukoba

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.