Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Sherehe za Uhuru: Wakuu wa nchi wamiminika Dar
Sherehe za Uhuru: Wakuu wa nchi wamiminika Dar
By Habari Tanzania | Published  12/9/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mwandishi Wetu

MARAIS wa nchi mbalimbali jana walianza kuingia kwa ajili ya sherehe za miaka ya Uhuru wa Tanganyika zinazofanyika leo katika uwanja wa Taifa jini Dar es Salaam.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana, baadhi ya marais hao na wawakilishi wa mataifa yaliyothibitisha kushiriki sherehe hizo, waliingia kwa zamu na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali na kuelekea mahali walikopangiwa kufikia.

Aliyekuwa wa kwanza kuingia ni Waziri Mkuu wa Lesotho, Pakalitha Mosisili aliyepokewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sofia Simba na kufuatiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Burundi, Marine Barampama ambaye pia alipokewa na Waziri Simba.

Kiongozi wa tatu kuingia alikuwa ni Rais Levy Mwanawasa wa Zambia aliyepokewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti na Utumishi, Hawa Ghasia na baadaye Rais Ahmed Abdallah wa Visiwa vya Comoro aliyepokewa na Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Dk Juma Ngasongwa.

Wakati marais hao wanaendelea kuingia na wengine wakitarajiwa kuingia mapema asubuhi leo, maandalizi ya mwisho ya sherehe hizo yalikuwa yakiendelea katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Katika Uwanja wa Mnazi mmoja ambao ulipangwa kutumika usiku wa kuamkia leo kulipua mafataki, kama ishara ya kumbukumbu ya kuteremsha bendera ya Mwingereza na kupandisha ya Tanganyika, ulikuwa umepambwa kwa nakshi mbalimbali.

Uwanja huo jana jioni ulikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wenye sare na makachero na milango yote ya kuingilia ziliwekwa mashine za kutambua vitu vyenye asili ya chuma.

Rais Jakaya Kikwete alitarajiwa kuwaongoza Watanzania katika ulipuaji wa fataki ambao ungeanza saa 5.30 hadi 6.00 usiku.

Vikundi vya burudani mbalimbali vilianza kutumbuiza katika uwanja huo jana jioni ikiwa ni pamoja na bendi za Shikamoo Jazz, DDC Mlimani Park, Msondo, Zanzibar Stars Taarab na mwanamuziki wa kizazi kipya, Juma Nature. Pia zilikuwapo ngoma za asili kutoka Arusha, Zanzibar, Dodoma na Chuo cha Sanaa Bagamoyo.

Leo shamrashamra za uhuru zinaendelea katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambako maonyesho ya ndege za kivita zitazokuwa zikiruka kuzunguka angani na kutoa salamu za heshima kwa mgeni rasmi, Rais Kikwete yatafanyika.

Rais Kikwete, leo anatarajiwa kulihutubia taifa kwenye Uwanja wa Taifa baada ya kupokea heshima za majeshi ya ulinzi na usalama na ndege tano za kivita zitakazokuwa zinapita angani.

Wananchi wametakaiwa kuwa watulivu na kutoogopa wakati ndege hizo zitakapokuwa katika tukio hilo.

“Watanzania wasishtuke hili ni jambo la kawaida na ili kuondoa hofu itapita ndege moja kwanza kisha zitafuatia nyingine, tunategemea zitakuwepo ndege tano,” Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Juma Akukweti alisema juzi akizungumza na waandishi wa habari.

Waziri huyo alisema sherehe hizo ambazo zitasindikizwa na mizinga 21, zitahudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo wananchi wa kawaida, viongozi wa ndani na nje ya nchi na kwamba Watanzania 50 waliozaliwa siku ya uhuru mwaka 1961 pia watashiriki.

Marais wengine waliotarajiwa kuhudhuria sherehe hizo ni Bingu wa Mutharika (Malawi), Armando Guebuza wa Msumbiji, Mwai Kibaki (Kenya), Yoweri Museveni (Uganda) na Paul Kagame (Rwanda).

Watu mbalimbali wamechangia sherehe hizo na kufikisha jumla ya Sh334,543,000.

Alisema maelekezo ya kudhibiti usalama wakati wa maadhimisho hayo yametolewa kwa vyombo vyote vya usalama hivyo wananachi wasiwe na wasiwasi juu ya suala hilo.

Barabara mbalimbali zinazoelekea katika hoteli za Kilimanjaro Kempinski, Movenpick, Holday Inn na Golden Tulip zilikuwa zinafungwa kadri wageni hao walivyokuwa wanaingia.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.