Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Afa akijaribu kupora kwenye gari la mizigo
Afa akijaribu kupora kwenye gari la mizigo
By Habari Tanzania | Published  12/8/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Eline Shaidi

JESHI la polisi mkoani Manyara limethibitisha kuuawa kwa mtuhumiwa wa sugu wa ujambazi aliyekuwa akiteka magari usiku katika barabara ya Arusha-Manyara.

Akithibitisha kuuawa kwa mtu huyo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Josephat Mwingira alisema mtu huyo aliuawa Desemba 6 usiku wa manane katika Kijiji cha Sinai wilayani Babati.

Alisema huyo aliyefahamika kwa jina moja la Rajab, alikutwa amelala barabarani mwili wake ukiwa umeharibika vibaya huku tochi yake aliyokuwa akiitumia katika uhalifu ikiwa pembeni.

Habari za kuaminika kutoka kwenye vyanzo vya habari zimeeleza kuwa alikuwa amedandia gari la mizigo kwa nyuma kwa lengo la kuingia kwenye gari hilo na kupora kabla ya kupigwa na utingo wa gari hilo na kudondoka chini.

Baada ya kuanguka chini gari lililokuwa nyuma yake lilimkanyaga na kusababisha kifo chake.

Polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi, huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mrara iliyopo mjini Babati.

Wakati huo huo, mchimbaji mmoja wa madini ya Tanzanite wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara, Juma Sudi (27), amekufa baada ya kuteleza kwenye ngazi na kutumbukia ndani ya mgodi.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani Manyara, Mwingira alisema mchimbaji huyo alianguka Desemba 6 saa 12
jioni katika mgodi uliopo kitalu D unaomilikiwa na Michael Pwnallm, raia wa Uingereza.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.