Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  MBUNGE ANAYEDAIWA KUONGOPA ELIMU YAKE:Jalada lafika ofisini kwa DPP
MBUNGE ANAYEDAIWA KUONGOPA ELIMU YAKE:Jalada lafika ofisini kwa DPP
By Habari Tanzania | Published  06/9/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
.Ilikuwa wakati wa kampeni za uchaguzi
.DCI asema tayari upelelezi umekamilika
 
MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) amepokea jalada la mbunge anayedaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu elimu yake wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.
 
Akizungumzia suala hilo ofisini kwake, Mkurugenzi wa Mashitaka, Geoffrey Shaidi, alithibitisha ofisi yake kupokea jalada hilo.
 
“Jalada limefika leo mezani kwangu… limepokewa ofisini Juni 6,” Shaidi alisema jana.
 
DPP ambaye hakuzungumzia undani wa jalada hilo, alisema ofisi yake italishughulikia na hakutaka kutaja jina la mbunge kwa wakati huu.
 
Awali, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, akizungumza na Uhuru alisema ofisi yake imekamilisha upelelezi kuhusu mbunge huyo na kuwasilisha jalada kwa DPP.
 
Manumba alisema ofisi yake ilipata taarifa za malalamiko kuhusu mbunge huyo na si kweli kwamba inawahoji wengine kadhaa.
 
Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kuwa wabunge kadhaa wamehojiwa na polisi kwa kughushi vyeti vikiwemo vya elimu.
 
Kutoka gazeti la Uhuru
Na Esther Mvungi

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.