Na Paulina David
MAHAKAMA€ Kuu Kanda ya Mwanza, imemuhukumu aliyekuwa askari la Jeshi la Polisi, E 7869 PC Ezra Kaira (35) kutumikia kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kumuua Mlima Mashaka kwa kumpiga risasi kichwani.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mfawidhi mwenye mamlaka ya kusikiliza kesi za Mahakama Kuu Federika Mgaya.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mgaya alisema kuwa, €mahakama hiyo imetoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa mshtakiwa huyo na watu wengine wenye tabia ya kuua raia bila kosa.
Awali kabla ya kutoa hukumu hiyo, Hakimu Mgaya alitoa nafasi kwa mshitakiwa huyo kutoa shufaa zake ili apunguziwe adhabu.
Akijetetea mahakamani hapo, mshtakiwa huyo aliiomba impunguzie adhabu kwa kuwa mke, mtoto na wazazi wake wanamtegemea.
Awali Wakili wa Serikali, Edwin Kakolaki aliimbia mahakama kuwa, Julai 13 mwaka 2001 usiku katika eneo la Nera na Barewa jijini Mwanza, askari huyo akiwa na wenzake wawili kwenye doria, walikutana na dereva teksi aliyewaambia amewaona watu kama majambazi eneo la Mlima wa Machemba.
Alisema askari huyo na wenzake walianza kuwafuatilia hadi walikoelekezwa, baada ya kuwaona walikimbia.
Mwendesha mashtaka huyo alisema kuwa, mshtakiwa na wenzake, waliendelea kuwafuatilia€watu hao hadi eneo la Mkanyeye, lakini walikimbia na kujificha kwenye jumba moja.
" Mara baada ya mshtakiwa na wenzake kufika huko, walikutana na mlinzi ambaye aliulizwa kuwa amewaona watu waliokimbia, aliwaonyesha na kufanikiwa kumkamata Mlima Mshaka na kumwamuru kulala chini," alisema na kuongeza kuwa:
" Mshtakiwa aliwaagiza wenzake watafute kamba ili wamfunge na kumpeleka kituoni, wakati wenzake wakitafuta kamba, walisikia mlio wa risasi na walipokwenda eneo la tukio walikuta Mlima ameuawa kwa kupigwa risasi ya kichwani."