Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Utatuzi wa kivuko Kigamboni 2008
Utatuzi wa kivuko Kigamboni 2008
By Habari Tanzania | Published  12/6/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mwandishi Wetu

HATUA za tahadhari za kuondoa uwezekano wa kuzama baharini kwa vivuko vyake vya Mv Alina na Mv Kigamboni zimeanza kuchukuliwa na serikali na matunda yake yanaweza kuanza kuonekana mwaka 2008

Katika hatua hizo, serikali imeandaa mpango wa muda mfupi utakaokamilika Mei mwakani, wakati wa muda mrefu unaotarajiwa kuzaa matunda baada ya miezi 15 kuanzia sasa. Mipango hiyo kwa pamoja itagharimu karibu Sh10 bilioni.

Wakati hayo yakielezwa, hali ya usafiri katika vivuko hivyo ni mbaya na jana wakazi wa Kigamboni walikaririwa na gazeti hili wakisema kuwa pantoni hizo zimekuwa zikiharibika mara kwa mara, hali ambayo inawatia wasiwasi juu ya usalama wa maisha yao wanapovitumia.

“Hii Serikali yetu inafanya utani na maisha ya watu. Ngoja siku moja lizame na wananchi wafe, ndipo wataheshimu umuhimu wa huduma hizi,” alilalamika Ally Abdallah, mkazi wa Kigamboni.

Baadhi ya watu walionekana wakitumia boti ndogo za watu binafsi kuvuka eneo hilo, huku watu wenye magari wakiwa hawajui la kufanya kutokana na boti hizo kutokuwa na uwezo wa kubeba magari.

Katika mpango wa muda mfupi, Serikali kupitia Wizara ya Miundombinu tayari imekwisha kuagiza injini mpya mbili za kivuko cha Mv Alina ambazo zitagharimu Sh800 milioni na zinatarajiwa kuingizwa nchini Mei mwakani.

Injini hizo za Mv Alina zitaingizwa na Kampuni ya Schottel GmH.Co. Kg ya Ujerumani, ambazo kwa mujibu wa wizara hiyo, zikifungwa, zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la usafiri kati ya Kigamboni na Magogoni.

Mpango huo wa serikali pia unahusu matengenezo ya kivuko cha Mv Kigamboni ambacho tayari zabuni yake imekwisha kutangazwa tangu Novemba 14 na gharama zake zitagharimiwa na Benki ya Dunia (WB).

Wakati mipango hiyo ikiwa ni ya muda mfupi, wizara pia tayari inaendelea kukamilisha taratibu za kuingiza kivuko kipya kikubwa kutoka Ujerumani ambacho kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 500, abiria 2,000 na magari madogo 60 kwa wakati mmoja.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Ufundi na Umeme wa Wizara ya Miundombinu, John Ndunguru, alisema kivuko hicho kitaingizwa nchini na Kampuni ya Neue Ruhrorter Schiff Swertf GmbH ya Ujerumani ndani ya miezi 15 ijayo.

Akizungumzia uingizaji kivuko kipya, ambacho nacho kitatoka Ujerumani, Ndunguru alisema amerudi juzi kutoka nchini humo ambako alikwenda kukiangalia.

Hata hivyo, Ndunguru alisema kivuko hicho hakitaingizwa nchini kizima, bali kitakuja vipande vipande na kitaunganishwa baada ya kuwasili.

"Najua watu hawataki kusikia maneno, lakini mpango wa kuboresha usafiri wa vivuko vya Kigamboni utagharimu si chini ya Sh10 bilioni," alisisitiza Ndunguru ambaye alikuwa Ujerumani kukagua kivuko hicho.

Kuhusu tukio la juzi la kuzima ghafla kwa kivuko cha Mv Alina, Ndunguru alisema taarifa alizopata ni kwamba, kivuko hicho kilizima kutokana na matatizo yake ya kawaida ambayo ni ya injini na kwamba ndiyo maana wameagiza injini mpya.

Wananchi wanaotumia usafiri wa vivuko kati ya Kigambo na Magogoni wamekuwa katika hatari kubwa ya kupoteza maisha na mali zao kutokana na ubovu wa vivuko vya sasa.

Tukio la mwisho ni la juzi ambalo Mv Alina ilikwama baharini na kufanya huduma za usafiri katika eneo hilo kutolewa kwa msaada wa kivuko cha Jeshi la Wanamaji (Navy) Kigamboni.

Katika miaka ya 80 kivuko kilichonunuliwa na serikali kwa ajili ya kutoa huduma katika eneo hilo, Unifloat, kilisababisha malalamiko makubwa baada ya kushindwa kumudu kazi hiyo baada ya kufanya kazi kwa siku chacha tu.

Kutokana na kushindwa kumudu kazi hiyo wananchi walitumia mitumbwi ya watu binafsi ambayo haikuweza kumudu kazi hiyo na kusababisha maafa


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.