Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mbowe aongea na watanzania mtandaoni
Mbowe aongea na watanzania mtandaoni
By Habari Tanzania | Published  12/5/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na HabariTanzania.com
*Awapongeza kwa uzalendo wao kujadili masuala ya kitaifa
 *Awaasa kutofanya masikhara na siasa wala viongozi
 *Watanzania walio mtandaoni wamjibu, wengine wamwuliza maswali kedekede
 
 
 Katika hatua ambayo imeonyesha kuwafurahisha watanzania watumiao mtandao wa intanet walio ndani na nje ya Tanzania, Mhe. Freeman A. Mbowe amejitokeza na kujisajili katika Mtandao mmoja na kutoa maoni yake kama watanzania wengine wafanyavyo.
 
 Hali hii imewafurahisha watanzania walio wengi kwani badala ya kuendelea kuongea mambo bila kuwa na mlengwa wa kuelekeza maswali yao na kero zao kwake wamempata kirahisi na kumwuliza au kumpa ushauri wao harakaharaka.
 
 Tarehe 2, Desemba 2006 Mheshimiwa Mbowe alijisajili katika www.JamboForums.com na kueleza hisia zake & shukrani kwa watanzania ambao wamekuwa wakichangia katika mijadala mbalimbali mtandaoni.
 
 Baadhi ya watanzania waliomhoji au kutoa shukrani zao wamempongeza Mhe. Mbowe kwa kutumia njia ya mtandao na kujiweka bayana. Wengine walionekana kutofurahishwa na kitendo chake kujiweka bayana wakidai kuwa inaweza kumwaribia jina.
 
 Maoni mbalimbali yametolewa na Mhe. Mbowe aliahidi kutoa majibu moja baada ya jingine (hasa yatakayoonekana ya msingi).
 
 Tunapenda kuungana na watanzania wenzetu kumshukuru Mhe. Mbowe kwa kuingia mtandaoni bila kujificha ili watanzania waweze kumwuliza maswali mbalimbali na tunamwomba asiwadharau au kuchukia pale atakapoulizwa maswali yanayoelekea kuwa na dhamira mbaya. Atambue wazi kuwa wanadamu hatufanani na lazima kuna wanaomuunga mkono na wasiomuunga mkono.
 
 Aidha ingependeza viongozi zaidi wa kitaifa wangetumia fursa hii ya mtandao kuweza kuwafikia wananchi mbalimbali kwani wanakuwa wanatoa dukuduku zao bila kificho na bila wasiwasi.
 
 Kupata kujua watanzania wamemwuliza maswali gani na amejibu nini Bofya hapa: www.JamboForums.com

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Anon)
    Rating
    Hapo lazima na JK au EL waje! Mi nina maswali ya kuwatwanga hawa...

    Sina mengi kwa Mbowe lakini kaonyesha ukomavu wa kisiasa. Wanaoogopa kuingia online ni wale wanaojua kuwa watabanwa sana na mambo yao mabovu yataanikwa hadharani!

    Well done Mbowe, well done JamboForums & all people in that forum. I like this kind of conversations online as am feeling free to ask any question!

    By the way, Mramba ameshajiuzulu?

    Regards
     
  • Comment #2 (Posted by Soames Phares)
    Rating
    Good one.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.