Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Magufuli awajia juu mameneja NHC
Magufuli awajia juu mameneja NHC
By Habari Tanzania | Published  06/8/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli,amesema kuwa atawafukuza kazi mara moja mameneja wa Shirika la Nyumba nchini (NHC) watakaobanika kuwa wabovu.

Alitoa tishio hilo jana wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa shirika mjini Morogoro.

’’Nitawafuatilia mameneja wanaolalamikiwa na watakaogunduliwa, watasimamishwa kazi,wengine nitawafukuza na kuwafikisha mahakamani’’ alisema.

Alisema baadhi ya mameneja wamekuwa wakiharibu sifa ya shirika hilo kwa kuwa wapokeaji wa rushwa kwa kuweka madalali kutafuta wateja wa kupanga katika nyumba za shirika hilo kwa ajili ya makazi na sehemu za biashara.

’’Kama kule Ilala wanaye dalali wao anaitwa Osama, madalali kama hawa wamekuw wakipokea hadi shilingi.

milioni 30 kwa nyumba za biashara na shilingi hadi milioni 8 kwa nyumba za kawaida za makazi, hii ni aibu, njia pekee ni kuitisha tenda na kutoa nyumba hizo kwa utaratibu,’’Alisema Magufuli.

Alisema mameneja hao iwapo watatumia njia bora kupangisha wapangaji wao kwa mujibu wa sheria wataweza kupata fedha nyingi ambazo zitawezesha kuimarisha maslahi ya shirika na hata kufanikiwa kuongezwa mishahara yao.

Alibainisha kuwa mameneja wamekuwa wakilalamikiwa sana kuhusika na rushwa hizo hivyo hawana budi kuacha mara moja mchezo huo kabla ya kuchukuliwa hatua hizo kali za kisheria.

’’Sitaki kuwafukuza watu kazi kama kule ujenzi,sitaki kumfukuza meneja hata mmoja na naahidi nitawalinda kama mtakuwa mnaonewa lakini kwanza mbadilike kuanzia leo,’’ alisisitiza Waziri.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.