Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Walemavu wagoma kuhamishwa kwa staili
Walemavu wagoma kuhamishwa kwa staili
By Habari Tanzania | Published  12/5/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Watanda barabarani kusubiri lolote
 
Operesheni yasimamishwa
 
Na Peter Orwa
 
MPANGO wa kuwaondoa wafanyabiashara walemavu, kwenye vibanda vilivyopo mtaa wa Lumumba, mjini Dar es Salaam, jana ulisimamishwa ghafla baada ya walemavu kukaa barabarani wakiwa tayari kugongwa na magari au kupigwa kwa mabomu ya kutoa machozi.
 
Meya wa Manispaa ya Ilala, Abuu Jumaa, alilazimika kusimamisha mpango huo baada ya kuona walemavu karibu 50 wakiwa wametanda kwenye makutano ya barabara ya Bibi Titi na Uhuru na kusababisha magari yaliyokuwa yakisafiri kwenye barabara ya Bibi titi kutoka uwanja wa ndege au eneo la Hoteli ya Peacock kushindwa kuendelea.
 
Kutokana na hali hiyo, Meya Jumaa alifika eneo la tukio na kujaribu kuzungumza nao, lakini alishambuliwa kwa kauli chafu, ambazo zilimfanya aondoke akiwa na baadhi ya viongozi wa walemavu.
 
Viongozi wao walikwenda kufanya kikao cha dharura na meya na baadaye, katibu wao wa uenezi, Abu Katesh aliwatangazia wenzake kwamba mpango wa kuwaondoa umesimamishwa.
 
Katesh aliwasili saa 3.00 na kuwatangazia msimamo huo kwa kuwasomea ulioandikwa kwenye karatasi.
 
Aliongeza kuwa wamefikia hatua ya makubaliano ya mandishi na si “ huruma ya mdomo”.
 
Kufuatia tangazo hilo, walemavu waliamua kuondoka barabarani kwa amani, huku wakitamba kwamba hatimaye walishinda vita, na kuhimizana waende wanywe chai nzito na vitafunwa safi kujipongeza.
 
Kitendo cha walemavu kukaa barabarani kilizuka ghafla saa 12.00 asubuhi na kudumu kwa saa tatu, ambapo licha ya kuombwa na polisi, walikataa kuondoka, wakisema walikuwa tayari kugongwa na magari au kupigwa kwa mabomu.
 
Baadhi yao walikuwa wamebeba mabango yasiyopungua saba na waliamua kukaa nayo barabarani wakati wengine walikuwa wamelala na kugalagala kwa kilio.
 
Vitendo hivyo ndivyo vilivyomfanya Meya Jumaa kuondoka na viongozi wa walemavu kwenda kufanya kikao cha dharura.
 
Wakati wote huo eneo hilo la barabara lilikuwa chini ya ulinzi wa Polisi, walioongozwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Masindoki Masindoki.
 
Leo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho wa notisi ya siku sita iliyowataka wahamishe shughuli zao Mtaa wa Lumumba.
 
Wakati sakata linaendelea, magari yote zikiwemo daladala, yalilazimika kupitia barabara za Lumumba, Nkurumah na mengine ya katikati ya jiji.
 
Lakini magari yaliyopita Barabara ya Uhuru yaliendelea na safari kama kawaida.
 
Akizungumzia sababu za mgomo huo, Mwenyekiti wa UWAWADA, Peter Gwikama, alisema walifikia hatua hiyo ya kufunga barabara kwa lengo la kutaka kumuona Rais Jakaya Kikwete ili wazungumze nao.
 
"Tunamtaka Rais Kikwete au Waziri Mkuu Edward Lowassa ndiye tuzungumze naye," alisema.
 
Gwikama alisema waliamua kuchukua hatua hiyo ili kupinga kuondolewa eneo hilo kwa nguvu kinyume na haki za binadamu.
 
“ Eneo la Mnazi mmoja tulipewa na Manispaa miezi minne iliyopita, na tumetumia fedha nyingi kujenga mabanda, lakini sasa Manispaa hiyo hiyo inatoa siku sita tuondoke twende Mchikichini. Hatua hiyo siyo ya kiungwana kwani uamuzi haujatushirikisha, " alisema.
 
Gwikama alisema wafanyabiashara walemavu kwanza wanataka kufanya mazungumzo na viongozi wa Manispaa na pia watataka fidia kwa kazi ambayo waliifanya ya kujenga vibanda Mnazi Mmoja, ili iwasaidie kulipa madeni mbalimbali ya kibiashara.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.