Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  K'njaro Stars yaisubiri Rwanda au Sudan
K'njaro Stars yaisubiri Rwanda au Sudan
By Habari Tanzania | Published  12/3/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Frank Sanga, Addis Ababa

MPINZANI wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars atafahamika leo kwa ajili ya mchezo wa robo fainali wa Kombe la Chalenji keshokutwaa.

Kilimanjaro Stars inayoongoza Kundi A kwa kufikisha pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu, itacheza robo fainali na mshindi wa pili wa Kundi C ambaye atajulikana baada ya mechi ya Uganda na Somalia.

Uganda, ambayo inaongoza Kundi C kwa kuwa na pointi sita wakati Somalia ambayo imefungwa mechi zote mbili za kundi hilo dhidi ya Rwanda na Sudan.

Uganda, inayofundishwa na Mjerumani Csaba Laselo inapewa nafasi kubwa ya kuishinda Somalia na kuongoza kundi C, hivyo kuikwepa Kilimanjaro Stars. Uganda inahitaji hata sare kuongoza kundi hilo.

Ikiwa na winga wake machachari, Danny Wagaluka bila shaka Uganda haitafanya makosa kupeleka kilio na kuwafunga virago Wasomali katika mchezo huo ambao utaanza saa kumi jioni.

Shughuli nyingie pevu katika kundi hilo itakuwa kati ya Rwanda na Sudan katika mchezo ambao utaanza saa
12:00 jioni.

Ikiwa na mshambuliaji wake, Abeid Mulenda, Rwanda itakuwa na kazi ngumu ya kuifunga Sudan inayocheza mpira wa kuvutia na kuelewana uwanjani.

Sudan na Rwanda zote zina pointi tatu, lakini Sudan ina idadi nzuri ya magoli hivyo matokeo yoyote ya sare yataifanya Sudan kukamata nafasi ya pili na kucheza na Kilimanjaro.

Rwanda inatakiwa kushinda mchezo wa leo ili ishike nafasi ya pili na kucheza na Kilimnjaro Stars.Wachezaji wengi wa Kilimanjaro wanaomba kucheza na Rwanda kuliko Uganda au Sudan zinazocheza mpira wa kuelewana, kuvutia na kibabe.

Kama ilivyo kundi A, katika Kundi C pia timu tatu zitafuzu kwani licha ya Uganda kufuzu kwa robo fainali, timu nyingine mbili zinazopewa nafasi kubwa ni Rwanda na Sudan.

Wakati huohuo, Ethiopia juzi usiku iliifunga Malawi bao 1-0 katika mchezo wa Kundi A na kuifanya ishike nafasi ya pili baada ya kumaliza mechi zake zote za kundi hilo.

Ilipata bao hilo dakika ya 42 lililofungwa na Dawti Mebruti na kuifanya ifikishe pointi sita huku Kilimanjaro Stars ikiongoza kwa kuwa na pointi tisa. Malawi ina pointi tatu wakati Djibout imeaga kwa kutokuwa na pointi yoyote.

Timu tatu za Kundi A, Kilimanjaro, Ethiopia na Malawi zimefuzu kwa robo fainali.Mechi za makundi zitamalizwa leo Jumapili na mechi za robo fainali zitaanza Jumanne kwa Kilimanjaro kucheza na mshindi wa pili wa Kundi C.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.