Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Aangua kilio kwa kuwa kibarua miaka 20 KCMC
Aangua kilio kwa kuwa kibarua miaka 20 KCMC
By Habari Tanzania | Published  12/3/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Ally Sonda, Moshi

MTUMISHI wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (KCMC), ameangua kilio mbele ya Katibu Mkuu wa Taifa wa Chama cha Watumishi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Ally Kiwenge wakati akiwasilisha kero yake ya kutopewa barua ya kutambuliwa kazini.

Mtumishi huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Devota, ambaye aliajiriwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tangu mwaka 1986, alimueleza Katibu Mkuu huyo kuwa katika muda wa miaka 20 sasa, hajapewa barua hiyo hali inayosababisha ajione kama kibarua.

Alitoa lalamiko hilo katikati ya wiki hii, kwenye Mkutano wa Wanachama wa Tughe na Wafanyakazi wa KCMC uliohutubiwa na Katibu Mkuu huyo wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani Kilimanjaro.

Alisema pamoja na kutokupewa barua hiyo, Serikali imekuwa ikimkata michango ya pensheni katika mshahara wake, hata hivyo fedha hizo, hafahamu zinakwenda wapi wakati wizara bado haijamtambua kwa barua kama mtumishi wake.

Akizungumza kwenye mkutano huo mara baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi ya Tughe,Tawi la KCMC, Kiwenge, alisema ni uonevu na aibu kubwa kwa maafisa waliohusika kumnyima mtumishi huyo barua yake ya kutambuliwa kazini.

Alisema mtumishi yeyote wa serikali anayefanya kazi bila ya kuwa na barua ya kutambuliwa, ajilinganishe na mtu aliyekalia kuti kavu ambalo linaweza kuvunjika wakati wowote na kumjeruhi au kusababisha kifo.

Kiwenge, amemuagiza Katibu wa Tughe Kilimanjaro, John Sanjo, kuorodhesha watumishi wote wa Serikali wakiwamo wa idara za kilimo na mifugo na hospitali ambao hawana barua za kutambuliwa kazini na kuwafikisha majina hayo makao makuu ya chama hicho kwa hatua zaidi.

Hata hivyo, aliupongeza uongozi wa KCMC, kwa kukubali kufungua Tawi la Tughe hospitalini hapo kwa manufaa ya wafanyakazi wake.

Awali katibu Mkuu huyo alifanya kikao na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambako alimshauri muajiri wake ambaye kuhakikisha kuwa kamati ya ajira inafanya vikao vyake kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

Alisema madhara ya Kamati hiyo kutofanya vikao ni pamoja na watumishi wengi kutokupandishwa vyeo, kutokurekebishiwa mishahara kwa wale wanaopanda vyeo kama ilivyo kwa watumishi wengi wa Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi ambao kwa zaidi ya miaka 15-20 hawajapandishwa vyeo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.