Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete amemtaeua Abeid Mwinyimusa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuanzia Novemba 28, mwaka huu.
Uteuzi huo uliotangazwa na katika taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, unaziba nafasi ya Ditopile Mzuzuri aliyejiuzulu hivi karibuni kutokana tuhuma za mauaji ya dereva wa daladala zinazomkabili.
Kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa huo, mwinyimusa alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mjini. Mwinyimusa ataapishwa na Rais Kikwete Jumatatu Desemba 4, mwaka huu.
Vile vile, siku hiyo, Kikwete atawaapisha Balozi Patrick Mombo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Edward Hosea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia Rushwa (Takuru).