Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kikwete asisitiza umuhimu wa masomo ya Kompyuta
Kikwete asisitiza umuhimu wa masomo ya Kompyuta
By Habari Tanzania | Published  06/7/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali haiwezi kuchagua kufundisha masomo ya kawaida tu katika shule bila elimu ya kompyuta kwa sababu taifa litakula hasara katika ulimwengu wa sasa.

Rais Kikwete alisema hayo mjini Zanzibar jana katika ufunguzi wa kituo cha Elimu Mbadala kilichopo Rahaleo kilichojengwa kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

’’Nimearifiwa pia kuwa mbali ya kusoma masomo ya kawaida lakini pia watajifunza elimu ya kompyuta, nawapongeza kwa jambo hili muhimu sana kwani katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia, kujifunza matumizi ya kompyuta hakuna mbadala,’’ alisema na kuongeza, ’’Ndiyo mwelekeo wa dunia ya leo na ndiyo hali halisi, hatuwezi kuchagua kufanya vinginevyo tutakula hasara.’’

Kituo hicho kitapokea watoto na vijana waliolazimika kukatisha masomo yao kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za umaskini, ndoa na ujauzito, hali ambayo inatoa fursa nyingine kwa vijana kujipatia elimu na kujiendeleza kimaisha.

Aliwasihi vijana watakaopata fursa ya kujiunga na kituo hiki waitumie nafasi hii ipasavyo kwa kuwa hiyo ni nafasi pekee ya kujijengea uwezo wa kujitegemea na kujikomboa kimaisha.

Alisisitiza kuwa katika karne hii ya 21 ambayo imetawaliwa na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, hatuna budi kuhakikisha kuwa watoto wanasoma katika mazingira bora yanayovutia kama yaliyopo katika kituo hicho.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.