Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wahujumu wabomoa majengo ya sekondari, Mbunge wa Kyela aja juu
Wahujumu wabomoa majengo ya sekondari, Mbunge wa Kyela aja juu
By Habari Tanzania | Published  11/30/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Brandy Nelson

UHARIBIFU mkubwa umefanywa na watu wasiojulikana wanaodaiwa kula njama na kuvunja majengo ya shule mpya ya Sekondari ya Mwaya iliyoko wilayani Kyela mkoani Mbeya na kusababisha masomo kusitishwa.

Mbunge wa Jimbo la Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, alisema jana jijini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akielezea tukio hilo alilodai kuwa ni hujuma na njama za watu wasiopenda maendeleo.

Dk Mwakyembe alisema kuwa uvunjaji huo wa shule iliyojengwa kwa nguvu za wananchi, umeathiri shughuli za kielimu kwenye shule hiyo kwa kuwa vifaa vyote na thamani zilizokuwemo kwenye ofisi za utawala vimeharibiwa na baadhi kuibwa.

Alisema watu hao walivunja madirisha, milango na walipoingia ndani waliendelea kuvunja kuta kwa kutumia vitu vyenye ncha kama vile shoka,nyundo na nyundo na kuvunja vunja samani za ofisi zilizokuwepo.

Mbunge huyo alisema, kamati ya shule hiyo kwa kushirikiana na wahandisi walifanya tathimini ya haraka na kugundua kuwa mali yenye thamani Sh5 milioni imeharibiwa na nyingine kuibwa.

Alisema kuwa tukio hilo sio la kwa kuwa wiki mbili zilizopita uvamizi kama huo ulifanyika kwenye shule hiyo kwa kuvunja makenchi kwenye vyoo vya wanafunzi na mabati kung'olewa ukiwemo msingi wa nyumba za walimu uliovunjwa kisha wahusika hao kutoweka.

Katika Mkutano na wakazi wa Mwaya aliwataka wawafichue waliohusika na njama hizo kwa kuwa wanawafahamu na wanaishi nao. Aliwataka watoe taarifa polisi ili waweze kunaswa vinginevyo uharibifu huo utakwamisha masomo kwa watoto wao.

Wakati wananchi wanatafakari hatima ya hujuma hiyo, mlinzi wa shule hiyo na wanakijiji wawili wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.