Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Muasisi amtaka Kikwete kutaja wauza 'unga'
Muasisi amtaka Kikwete kutaja wauza 'unga'
By Habari Tanzania | Published  11/30/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Ally Sonda

MUASISI wa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), amemtaka Rais Jakaya Kikwete kufuata nyayo za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutangaza majina ya watu wanaodhaniwa kuwa ni wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini.

Mzee Bomba, mkazi wa Mabogini, alionya kuwa licha ya Rais Kikwete kupendwa na watanzania wengi, serikali yake inaweza kuonekana ya ajabu endapo haitawataja na kuwafikisha mahakamani wanaotuhumiwa kufanya biashara hiyo haramu.

Bomba ambaye aliwahi kuwa dereva wa Waingereza wakati wa vita kuu ya Pili ya Dunia, alisema kutotajwa kwa majina ya wafanyabiashara hao na kuwafikisha mahakamani unawapa mashaka makubwa wananchi.

Alisema visingizio vinavyotolewa na vyombo vya dola likiwamo Jeshi la Polisi kuwa linafanyia kazi majina ya wafanyabiashara hao, hazina msingi kwa kuwa watu hao walipaswa kufanyiwa uchunguzi wakiwa mbaroni.

" Polisi wakisikia mtu fulani anauza bangi wanavamia nyumba yake na kumkamata na hata wakipekuwa nyumba na wakakosa hiyo bangi bado watamchukua hadi kituoni na kumsweka rumande ... sasa mbona hao wanaouza dawa hawaswekwi rumande? " alihoji.

Alisisitiza kuwa, sheria inayotumika kuwabana wauza mirungi, bangi na gongo isitumike kwa wanyonge bali iwaadhibu wakosaji wote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Amempongeza Mbunge wa Viti Maalum (Vijana-CCM), Amina Chifupa Mpakanjia kwa ujasiri wa kuamua kulisaidia Jeshi la Polisi kuwanasa wauza unga na kumuomba Kikwete kumlinda baada ya kuonyesha kukerwa na vitendo hivyo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.