Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Hakimu akataa ombi la kukamatwa Tibaigana
Hakimu akataa ombi la kukamatwa Tibaigana
By Habari Tanzania | Published  11/30/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Tausi Ally

HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Neema Chusi, jana alikataa ombi la kutaka kukamatwa kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana, ili akatoe ushahidi mahakamani hapo.

Ombi hilo liliwasilishwa na Mkazi wa Kinondoni ‘A’ jijini Dar es Salaam, Stanley Damgoba (52), anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mali yenye thamani ya Sh7 milioni.

Damgoba aliiomba mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata Kamishna Tibaigana, baada ya kushindwa kutokea mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hiyo kwa mara ya tatu sasa.

Mtuhumiwa pamoja na wenzake wanne wanakabiliwa na kesi ya wizi.

Akikataa ombi hilo, Hakimu Chusi alisema kuwa mtuhumiwa huyo ndiye aliyemuomba Tibaigana apelekwe mahakamani hapo kutoa ushahidi katika kesi hiyo na siyo kwa amri ya mahakama.

Chusi alimtaka mshitakiwa huyo kutumia kila mbinu kumshawishi Tibaigana afike mahakamani hapo kutoa ushahidi na kwamba mahakama itakachomsaidia ni kutoa samansi ya kumuita Kamanda huyo mahakamani na si vinginevyo.

Alisema iwapo mshitakiwa huyo atashindwa kumfikisha Tibaigana mahakamani na kusimama kama shahidi wake hadi Desemba 12, atalazimika kufunga ushahidi kwa kuwa washitakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo wanalalamika kuwa wanacheleweshwa.

Washitakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni mlinzi na mkazi wa Mbezi Beach, Michael Daniel (25) na fundi mwashi, Cornel Ernest (37) wote wakiwa wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama na kuiba.

Ilidaiwa na upande wa mashitaka kuwa Mei 18, mwaka jana katika eneo la Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao waliiba luninga moja, deki za DVD mbili, deki mbili za video, kamera ya video moja, kamera ya digital moja, meza tatu za simu, deki moja ya VCD pamoja na redio tatu vyote vikiwa na thamani ya Sh7 milioni mali ya Dk Amza Mugula.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.