Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wanakijiji mpaka wa Tanzania na Uganda wamkataa mwenyekiti wao
Wanakijiji mpaka wa Tanzania na Uganda wamkataa mwenyekiti wao
By Habari Tanzania | Published  11/29/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Lilian Lugakingira

WAKAZI wa Kijiji cha Bugango Kata Kakunyu wilayani Missenye, wamekataa kuongozwa na mwenyekiti wao, Sofia Mbani kwa madai kuwa, anaishi nchini Uganda badala ya Tanzania.
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti wakazi hao walidai kuwa, tangu achaguliwe mwaka juzi kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho, amekuwa akiishi nchini humo.

Kutokana na kijiji hicho kuwa mpakani mwa Tanzania na Uganda, wakazi hao wamedai mwenyekiti huyo amekuwa akilala nchini humo na kuja kazini katika ofisi ya kijiji asubuhi na jioni kurejea nyumbani kwake.
Waliendelea kudai kuwa, kutokana na hali hiyo hawawezi kuendelea kuongozwa na mwenyekiti huyo badala yake, wanaomba ridhaa ya kuchagua mwingine.

Akizungumzia madai hayo, mwenyekiti huyo alisema kuwa anaisi kuwa huenda wakazi hao hawamtaki baada ya kusambaa kwa kwa taarifa kuwa ameshirikiana na uongozi wa Ranchi ya Missenye kuwanyang’anya ardhi yao .
Naye Katibu Tarafa wa Missenye Abas Ngilwa, alisema mwanzoni mwenyekiti huyo, alikuwa akiishi Tanzania, lakini kutokana na marekebisho ya mpaka mpya kati ya Tanzania na Uganda yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka 2003, shamba na nyumba yake vilirudi nchini humo .

Kwa mujibu wa Ngilwa, baada ya kuzuka kwa malalamiko kuhusiana na mwenyekiti huyo kuishi Uganda, alilazimika kutafuta nyumba ya kupanga kijijini hapo ambako hadi sasa anaishi.
Mwenyekiti huyo alichaguliwa na wakazi hao kushika wadhifa huo wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka juzi.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.