Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mgambo waomba mabomu kudhibiti wamachinga Dar
Mgambo waomba mabomu kudhibiti wamachinga Dar
By Habari Tanzania | Published  11/29/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Salhim Shao
MGAMBO wa Jiji la Dar es Salaam, wameomba waruhusiwe kutumia mabomu ya machozi katika zoezi la kuwaondoa wamachinga mitaani.

Wakizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Patrick Tsere jana, mgambo hao walisema walimuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, awaruhusu kutumia mabomu ya machozi wakati wakipambana na wamachinga.

"Tunapokwenda kufanya kazi ya kuwaondoa maeneo kama ya Kariakoo tunazingirwa na raia na kulazimika kuacha kazi hiyo kwa kushindwa kuwatawanya," alisema Damiani Mpangala, mmoja wa mgambo hao wa Manispaa ya Ilala.

Mgambo hao wa jiji walisema wanaposhambuliwa au kuzuiwa kufanya kazi zao na raia wenye hasira, hulazimika kuondoka kwani iwapo watatumia silaha za moto wanazopewa, madhara yake yanaweza kuwa makubwa.

Pia walilalamikia tabia ya viongozi wa serikali ambao wamekuwa wakiwaingilia pindi wanapowakamata watuhumiwa. "Tunakamata mtu baadaye anakuja kiongozi na kutaka tumwachie wakati amevunja sheria, inaumiza sana," alisema.

Walitolea mfano katika operesheni waliyokuwa wakifanya ya kuondoa vibanda katika maeneo ya jiji, ambako baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwataka waache baadhi ya vibanda na kuwaonyesha vingine vya kubomoa.

"Suala hili limefanya tuonekane tunafanya kazi kwa upendeleo na hivyo kujengewa chuki na watu, tunataka kama tunafanya kazi tusiangalie sura, vinginevyo hata heshima ya serikali inapungua kwa watu," alisema mgambo mwingine, Khalfan Kimaro.

Mkuu wa wilaya ambaye alikuwa amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro katika mkutano huo, alisema amepokea masuala yote waliyomweleza na kuwa atafikisha kwa watekelezaji ili yafanyiwe kazi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.