Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Bunge A Mashariki katika hati hati
Bunge A Mashariki katika hati hati
By Habari Tanzania | Published  11/27/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Claud Gwandu, Arusha

BUNGE la Afrika Mashariki (EALA) huenda lisizinduliwe mwishoni mwa wiki hii kama
ilivyopangwa endapo walalamikaji katika kesi ya kupinga uteuzi wa wabunge wa bunge hilo kutoka Kenya watashinda katika hukumu ya kesi hiyo itakayotolewa leo.

Kesi hiyo imefunguliwa na walalamikaji 12 wakiongozwa na Profesa Peter Anyang Nyong, ambao pamoja na mambo mengine wanapinga utaratibu uliotumika katika kupata wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Kenya.

Baada ya malumbano makali ya kisheria ya siku mbili kutoka kwa wakili wa walalamikaji, Mutula Kilonzo na upande wa utetezi ukiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Amos Wako, Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Moijo Ole Keluwa, aliahirisha kesi hiyo Jumamosi jioni na kutangaza kuwa hukumu yake itatolewa leo.

Wakati Kilonzo kwa niaba ya wateja wake akidai kuwa hakuna uchaguzi uliofanyika nchini humo, Wako naye kwa upande wa serikali alidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza malalamiko hayo na kwamba walalamikaji hawana hoja.

Akizungumza baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Msajili wa Mahakama ya Afrika Mashariki, Dk John Ruhangisa, alisema kuwa ikiwa walalamikaji watashinda, basi Bunge lililopangwa kuzinduliwa Novemba 29, mwaka huu litaahirishwa.

"Kwa mujibu wa mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bunge huzinduliwa kwa spika mpya kuapishwa kwanza lakini kama walalamikaji
watashinda, uchaguzi wa spika hautafanyika kwa sababu spika anatakiwa kuapishwa mbele ya Bunge zima.

“Kumbukeni hili ni Bunge la Afrika Mashariki likiwa na wabunge tisa kutoka kila nchi
mwanachama hivyo kama uchaguzi wa wabunge kutoka Kenya utatenguliwa na mahakama, idadi haitakuwa imetimia hivyo kulazimisha Bunge kuahirishwa,” alisisitiza Dk Ruhangisa.

Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Katibu wa Bunge la Kenya, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Msajili wa Mahakama ya Afrika Mashariki Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Makamu wa Rais wa Kenya ambaye ni mkuu wa shughuli za serikali katika Bunge la
nchi hiyo na Dk Mukhisa Kituyi ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha NARC-Kenya.

Kesi hiyo ya aina yake inasikilizwa na majaji watano wa mahakama ya Afrika Mashariki ambao ni Jaji Joseph Mulenga, Jaji Joseph Warioba, Jaji Augustine Ramadhan, Jaji Kasenga Mulwa chini ya Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Ole Keluwa.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.