Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Majambazi watawanya maharusi shereheni
Majambazi watawanya maharusi shereheni
By Habari Tanzania | Published  11/27/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mussa Juma, Arusha

MAJAMBAZI sita wakiwa na bunduki za aina mbali mbali, juzi usiku wamevamia kituo cha mafuta cha Njake, kilichopo Mto wa Mbu wilayani Monduli na kupora mamilioni ya fedha baada ya kupiga risasi kadhaa hewani zilizosababisha pia kuvunjika kwa harusi iliyokuwa inafanyika jirani na eneo hilo.

Katika tukio hilo la aina yake, mamia ya watu waliokuwa wakihudhuria harusi ya mtangazaji wa kituo cha Radio 5 cha Arusha, Willy Cosmas, walilazimika kukimbia katika ukumbi wa starehe wa Twiga uliopo jirani na kituo hicho kunusuru maisha yao.

Tukio hilo lililothibitishwa na polisi, lilitokea majira ya saa 2:15 usiku, muda mfupi baada ya maharusi kuingia ukumbini.

Meneja wa Kituo cha Radio 5 ambaye alikuwa ni mmoja wa waalikwa katika sherehe hizo, Dionis Moyo, alisema baada ya mirindimo hiyo ya risasi, watu wote walitawanyika na bwana harusi alitoweka na akaonekana baada ya robo saa, baada ya tukio hilo, akitokea mafichoni huku bibi harusi akiwa amejificha chini ya moja ya magari ya waalikwa.

"Hali ilikuwa mbaya sana, mimi binafsi nilikuwa sijawahi kusikia bunduki zinapigwa karibu yangu...wote tulitawanyika na kuacha ukumbi wazi na baada ya nusu saa tulilazimika kurejea Arusha," alisema Moyo.

Alisema hata hivyo, hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa katika tukio hilo. Moyo alisema bibi harusi, Cathelini Pisa, ambaye ni mwalimu katika Chuo cha Ufundi Mto wa Mbu akiwa na mavazi ya harusi, alijificha chini ya gari lao lililokuwa limekodishwa kutoka Arusha.

Moyo alisema, majambazi sita, watatu wakiwa na bunduki aina ya Sub Mashine Gun (SMG), mara walipovamia eneo hilo walipiga risasi kadhaa hewani na ndipo waliiingia kwa mtunza fedha na kuchukua kiasi kikubwa cha fedha.

Hata hivyo, hadi kufikia jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Matei Basilio alisema bado alikuwa hajapata kiasi cha fedha kilichoporwa na taarifa sahihi juu ya tukio hilo.

"Hapa mimi nilipigiwa simu jana usiku kuhusiana na tukio hilo na nimemuagiza afisa wa polisi pale mto wa mbu aniletee taarifa kamili," alisema Basilio.

Katika siku za hivi karibuni matukio ya uvamizi katika vituo vya mafuta yamerejea tena kwani mwishoni mwa wiki iliyopita, majambazi walivamia kituo cha mafuta cha Mount Meru Posta.

Katika tukio hilo, majambazi hao hata hivyo walidaiwa kutumia silaha za jadi na baruti kutawanya watu na kutishia wauzaji wa mafuta kabla ya kutoweka na fedha.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.