Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Safari nyingi za Rais Kikwete zaleta maneno
Safari nyingi za Rais Kikwete zaleta maneno
By Habari Tanzania | Published  11/26/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Mwandishi Wetu

Takriban mwaka mmoja wa utawala wake, Rais Jakaya Kikwete, pengine anaweza kuwa Rais aliyetumia muda mwingi safarini kuliko wengine waliomtangulia tangu aingie madarakani.
 
Habari ambazo Mwananchi Jumapili imezikusanya kutoka vyanzo mbalimbali zinaonyesha kwamba, safari alizozisafiri nje ya nchi peke yake zikiachwa zile za ndani, hivi sasa anakaribia kuzidi miezi miwili akiwa safarini yaani zaidi ya siku 74 katika mwaka. Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha pia kwamba miongoni mwa safari hizo Rais amekuwa akiambatana na ujumbe mzito wa maafisa wa serikali ambao hutumia fursa mbalimbali katika safari hizo.
 
Miongoni mwa fursa hizo ni kufikia katika mahoteli ambayo uchunguzi unaonyesha yanalipiwa gharama si chini ya dola za kimarekani 1500 kwa siku. Pia katika safari hizo maafisa hupanda ndege daraja la kwanza ikichukuliwa mathalani safari moja ya Marekani, aliyoambatana na maafisa wa serikali na wadau mbalimbali zaidi ya 50, gharama zinaonyesha kuwa za juu ikilinganishwa na kama maafisa hao wangelitumia madaraja mengine.
 
 Suala la safari hilo ambalo kwa upande mmoja, linaonekana kuwa muhimu kwa maendeleo ya taifa hasa kutokana na ugeni wa rais katika wadhifa na mabadiliko ya sera za nje, bado limeonekana kuwa mzigo kwa taifa. Katika kipindi cha miezi 11 iliyopita, mathalani Rais Kikwete aliweza kusafiri katika maeneo mbalimbali ya dunia jambo ambalo halionekani kuwa kama suala zito.
 
 Kwa mfano kati ya Januari 19-25, mwaka huu rais alikwenda Khartoum, Sudan kuhudhuria mkutano wa AU, na baadaye Machi 23, akawa na ziara ya siku moja ya kiserikali kujitambulisha Kigali, Rwanda.

Kabla ya hapo Machi 22 akawa na ziara ya siku moja kujitambulisha Kampala, Uganda. Machi 24, akawa na ziara ya kiserikali kujitambulisha Nairobi, Kenya. Aprili 19-20, akasafiri kwenda kujitambulisha Lesotho na Swaziland na baadaye Aprili 21-22 , akaenda kujitambulisha Maputo, Msumbiji. Aprili 28, akaenda kujitambulisha Harare na Bulawayo, Zimbabwe. Aprili 6, akawa na ziara ya kujitambulisha Gaborone, Botswana. Aprili 10-12, kujitambulisha Windhoek, Namibia. Aprili 7-9, safari ya kikazi na kujitambulisha Pretoria, Afrika Kusini. Mei 12, akawa na ziara ya kiserikali ya wiki mbili kwenda Uganda ambako alikaa Mei 13, na kisha kuondoka kwenda Arabuni Mei 15, Ufaransa Mei 16-19 na Marekani Mei 21-26. Mei 31-Juni 3 akahudhuria World Economic Forum, Capetown Afrika Kusini. Julai 4-akahudhuria mkutano wa AU, Banjul Gambia. Julai 10-32, 2006 Capetown Afrika Kusini , kuhudhuria mkutano wa viongozi wa serikali ulioandaliwa na kampuni ya Microsoft ya Marekani.
 
Baadaye Julai 20 akahudhuria mkutano wa Leon Sullivan Summit Abuja, Nigeria. Julai 21 -22, akaenda kuchunguzwa afya Berlin Ujerumani. Agosti 19-20 akahudhuria mkutano wa SADC, Maseru, Lesotho. Agosti 21-22 ziarani ya kiserikali Luanda, Angola. Septemba 12- Havana Cuba maandalizi ya kikao cha NAM. Septemba hiyo hiyo lakini 15, alipita Madrid, Hispania kwenye Uwanja wa Mpira- Real Madrid. Septemba 15 -18, 2006 Havana Cuba, Mkutano wa NAM. Septemba 19-25 - akahudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Muda kidogo baada ya hapo akabakia nchini, lakini baadaye mwishoni mwa Oktoba mwaka huu akaenda ziara ndefu ya Mashariki ya kati ambako alikuwako kwa zaidi ya siku 14. Jana alihitimisha ziara yake nchini Uganda kwa Mwaliko wa Rais Museveni, na kufanya idadi ya siku alizotumia katika safari kuzidi 73. Awali Septemba mwaka huu,

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alimtaka Rais Kikwete kupunguza safari zake za nje ya nchi, badala yake atulie nchini kushughulikia matatizo ya kiuchumi yanayowakabili wananchi, likiwamo suala la umeme.
 
Profesa Lipumba, alieleza kuwa manufaa ya safari za Rais Kikwete kiuchumi ni ndogo ukilinganisha na gharama anazotumia. "Marekani amekwenda mara mbili, eti anakwenda kuitangaza Tanzania na kuwakaribisha wawekezaji.., utavutiaje wawekezaji wakati hauna umeme?" alihoji Profesa Lipumba. Akichambua hali ya uchumi ilivyo, alisema tangu Rais Kikwete aingie madarakani, ukali wa maisha na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu nchini umeongezeka kwa ari, kasi na nguvu mpya.
 
Akizungumzia suala hilo katika Hotuba yake ya Oktoba mwaka huu Rais Jakaya Kikwete alielezea mafanikio makubwa aliyoyapata katika miongoni mwa ziara hizo ikiwa ni pamoja na kuingia mikataba mbalimbali yenye faida na manufaa kwa jamii ya kitanzania. Alisema hakuna haja ya kuhoji ziara zake wakati kinaeleweka anachokwenda kukifanya kuwa dhahiri ni kwa manufaa ya jamii ya kitanzania.
 
Kauli hii ya kupigia debe mafanikio ya safari za Rais imewahi kutolewa siku za hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro, akisema kuwa ziara hizo zina mafanikio makubwa kwa nchi bila kuyaonyesha mafanikio hayo waziwazi. Dk. Migiro kwa wadhifa wake amekuwa pia akiandamana na rais katika safari mbalimbali duniani jambo linalofanya kauli yake ya utetezi wa safari za rais kubakiza maswali mengi kuliko majibu.
 
Waziri mwingine anayeungana na Dk. Migiro kupigia upatu safari za Rais ni Basil Mramba, Waziri wa (Viwanda na Biashara) ambaye naye pia kwa wadhifa wake wa sasa na ule wa zamani (Waziri wa Miundombinu) amekuwa akinufaika na safari hizo mara kadhaa. Kwa namna moja ama nyingine safari hizi zinaweza kuwa kikwazo katika majukumu ya ndani ya Rais na hasa suala la mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar, tatizo linaloonyesha kubakiza nafasi ya rais pekee ili kupata tiba na sio mtu mwingine.
 
Kauli za kukinzana kati ya viongozi waandamizi wa CCM na wale wa Chama cha Wananchi (CUF) zimeonesha kuwa pande hizo mbili hazina malengo ya kutatua tatizo lililopo na anayeweza kutumia nguvu zake binafsi ni Rais lakini naye anaonekana kuwa kimya, jambo linaloweza kupata jibu rahisi; kutingwa na majukumu aliyonayo na hizi safari za mara kwa mara nje ya nchi.
 
Vile vile, wachambuzi wa masuala ya siasa na utawala wanahusisha safari hizi, pamoja na ukubwa wa Baraza la Mawaziri la Rais Kikwete kama vikwazo vya ukuaji wa uchumi. Baraza la Kikwete lina mawaziri 60, na idadi hii ni kubwa kuliko mabaraza yote ya mawaziri yaliyowahi kuwepo nchini tangu kupatikana uhuru mwaka 1961. ends

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.