Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wanajeshi wapiga wananchi Dar
Wanajeshi wapiga wananchi Dar
By Habari Tanzania | Published  11/26/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mwandishi Wetu

ASKARI wanaodhaniwa kuwa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao idadi yao haikuweza kufahamika wamevamia eneo la Kigamboni, Dar es Salaam na kupiga watu ovyo na kusababisha shughuli za uchumi na kijamii kusimama kwa muda.

Tukio hilo lilitokea juzi Ijumaa jioni kwa kuhusisha askari hao ambao baadhi yao walikuwa wamevalia sare na wengine wakiwa katika nguo za kiraia. Katika vurugu hizo ambazo zilidumu kwa dakika takriban 10, zilisababisha askari hao kupiga waendesha daladala, teksi na kusababisha majeruhi ambao nao idadi yao haijafahamaika mara moja.

Watu walioshuhudia tukio hilo waliiambia Mwananchi Jumapili kwamba, askari hao walitoka kambi ya JWTZ, Kikosi cha Wanamaji (Navy)katika eneo hilo la Kigamboni ambao walipiga watu kwa mikanda kisha pia wakapora mali.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, eneo lililoathirika zaidi na ghasia hizo za wanajeshi ni kituo cha mabasi cha Feri, ambacho kipo karibu mita 200 kutoka katika kambi hiyo. Hali hiyo iliwafanya baadhi ya madereva wa daladala na watu wengine waliokuwa na magari kujificha chini ya uvungu wa magari yao kama hatua ya kujinusuru.

“Tulikuwa tunakunywa kahawa kama kawaida, mara ghafla tukaona watu wakikimbia kutoka huku na kule, na kwa sababu hatukujua nani alikuwa akipiga watu tuliamua kukimbia kwenda tuliko ona ni salama,” alisema mtu mmoja aliyekumbwa na tukio hilo. Kwa mujibu wa mashuhuda, vurugu hizo ambazo zilikiwsha dakika kumi baadae baada ya polisi kuarifiwa na kufika katika eneo la tukio, zilisababisha maduka na vioski vyote vya maeneo ya karibu kufungwa.

Baada ya polisi kufika katika magari mawili aina ya Landrover Defender, watu walikusanyika kwa tahadhari na kuanza kulalamikia hatua hiyo ya wanajeshi kufanya vurugu hizo. Kwa muda, hakukuwa na usafiri wa daladala wala taksi wa kubeba abiria kutoka Tuangoma, Tungi, Mjimwema, Kibada kwenda maeneo mengine ya Kigamboni.

“Tutachukua hatua zinazofaa kulinda nafsi zetu,” alisema mtu mmoja kauli ambayo iliwafanya polisi kuwa makini kutaka kujua nani alikuwa akipanga kupigana na wanajeshi hao.

Mwananchi Jumapili ilishuhudia wananchi wakiwa na hasira kutaka kujua kama polisi walifika katika eneo la tukio kutaka kuwalinda wao au kuwalinda wanajeshi hao. Kumekuwa na hali ya kutoelewana kati ya wavuvi na askari wa Navy kutokana na mara kwa mara boti zao kuonekana katika eneo la baharai karibu na mji wa Kigamboni.

Chanzo kingine kiliongeza kwamba, Jumatano wiki iliyopita, mtu aliyedhaniwa kuwa ni mwanajeshi wa Navy alipigwa na wavuvi kwa kumtuhumu kwamba alikuwa ni mwizi na kwamba ndiye aliyepanga tukio hilo la Ijumaa. Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Emmanuel Kandihabi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akasema Afisa Upelelezi wa Mkoa (RCO)alikuwa katika eneo la tukio kupata taarifa za kina. Kwa mujibu wa Kamanda Kandihabi, afisa huyo alikuwa katika timu ya pamoja na baadhi ya maafisa wa JWTZ ambao walikuwa Kigamboni.

Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Profesa Juma Kapuya alithibitishia Mwananchi Jumapili kuhusu kutokea kwa ghasia hizo na kusema tayari kulikuwa na maafisa ambao walikuwa wakifuatilia suala hilo kwa karibu. “Wapo maofisa wanalifanyia kazi suala hilo, wakishaniletea taarifa nitaweza kuzungumza kwa sasa sina taarifa za kutosha akuhusu suala hilo,” alifafanua Profesa Kapuya.

Huu ni mfululizo wa matukio ya askari wa Navy kupambana na wananchi, mara ya kwanza askari hao waliwahi kuwapiga wananchi wakiwa katika kipigo walichokipa jina la ‘Kuku’. Naye Salma Said anaripoti kutoka Zanzibar kuwa askari Polisi wawili wamejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa kwa marungu pamoja na ngumi katika kituo cha Polisi Fuoni na Askari wa Kikosi Maalumu cha Kufuatilia Magendo (KMKM).

Tukio hilo lilitokea majira saa 9:30 katika Kituo cha Polisi Fuoni Mkoa wa Kusini Unguja wakati Askari Polisi walipokuwa kazini waliposimamisha gari ya KMKM yenye usajili namba KM 126 iliyokuwa imepakia magogo ya miti ikitokea shamba kuelekea Mjini. Baada ya kusimamishwa na Polisi wa zamu Askari waliokuwepo ndani ya gari hilo la KMKM walishuka kwenye gari hilo zaidi ya 20 wakiwa na sare zao za kazini na wengine wakiwa wamevalia nguo za kawaida walianza kutoa kipigo kwa askari waliokuwepo karibu na wengine na kuwajeruhi wawili na wengine kujaribu kuwahami wenzao, lakini hawakufua dafu kutokana na KMKM waliokuwa wengi pamoja na magongo.

Askari hao wa KMKM walitumia magongo na ngumi kwa kuwapiga askari polisi waliopo zamu na huku magari yaliokuwa yakienda mjini na yaliokuwa yakitoka shamba kulazimika kusimama kutokana gari la KMKM kusimamishwa kati kati ya barabara.

Waliojeruhiwa ni Abass Shamna na Mwinyi Suleiman ambao wamekimbizwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kupatiwa matibabu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Amini Mhamba ameliambia Mwanananchi kwamba tukio lililotokea halipo katika eneo lake hivyo nimtafute Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi. “Mimi nipo mjini nimo ndani ya gari na hilo tokeo mpigie simu Kamanda wa Mjini sio mimi” alisema kwa simu Kamanda wa Kusini.

Alipoulizwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban pia alimtupia mzigo Kamanda mwenzake na kusema yeye hahusiki na tukio hilo kwa vile sio Mkoa wake. “Sawa lakini mpigie simu Kamanda wa Kusini kwa sababu hilo ni eneo la Kusini sio mimi” alisema Kamanda Bakari Walioshuhudia tukio hilo walisema walisema kwamba baada ya kushuka kwa kundi la Askari wa KMKM baadhi ya Askari wa Polisi waliokuwepo ndani ya kituo cha polisi cha Fuoni waliwakimbilia askari wenziwao na kujaribu kuwanusuru na kipigo kutoka kwa askari wa KMKM lakini walishindwa kutokana na wenziwao kuwa na silaha za kienyeji za magongo na kutumia mateke na ngumi.

 “Ahh tunaelekea hospitali kwa sababu tumeumia sana sijui ilikuwaje lakini naona hali tunapigwa tu” alisema mmoja wa majeruhi hao


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.